BURIANI KAKA YANGU MAALIM SEIF SHARIF HAMAD.
SEHEMU YA NNE: KUCHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA TAIFA NA MAALIM SEIF KATIBU MKUU WA CUF
Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, 28 Februari 2021
Niliporejea nchini mwaka 1998 kutoka Helsinki niliendelea na shughuli za utafiti na ushauri wa mambo ya uchumi nchi za nje. Miongoni mwa shughuli nilizofanya ilikuwa ni pamoja na kwenda Swaziland kuishauri Wizara ya Fedha ya nchi hiyo namna ya kuimarisha sera zake, kwa lengo la kukuza uchumi na kuwa na utulivu katika uchumi mpana. Aidha nilifanya ushauri kama huo kwa Wizara ya Fedha, nchini Namibia.