Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mazungumzo ya watu wa diniView attachment 1719324
IMG-20210306-WA0024.jpg
 
kiumbe anayefahamika kama Armadillo. Huenda wengi wetu hatumfahamu kiumbe huyu kwa sababu tu haonekani katika maeneo yetu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Armadillo hupendelea kuishi katika maeneo yenye joto na unyevunyevu. Wanyama hawa wanajulikana kwa miili yao midogo yenye rangi ya hudhurungi (zambarau) na mkia mrefu na mgumu, kichwa kirefu, macho madogo meusi, masikio marefu yaliyoelekea juu na miguu minne; miwili mbele na miwili nyuma.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kichwa cha Armadillo kinafanana kidogo na panya, lakini wenyewe wanashabihiana na Kakakuona.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wanyama hawa wanasifika kwa tabia yao ya kuchimba mashimo kwa kutumia kucha za miguu yao ya mbele na kisha kuingia ndani yake ili kujilinda na wanyama wakali.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya viumbe, kuna takriban aina 20 za Armadillo na aina zote hizo zinapatikana katika nchi za Amerika ya Kusini na Kaskazini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Armadillo hulazimika kutafuta maeneo ya udongo wenye kichanga ili kupata wepesi wa kuchimba na kujipatia chakula chao pamoja na sehemu ya kulala.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chakula na uzazi

Katika chakula, Armadillo hula wadudu jamii ya amfibia au reptilia kama konokono na funza kwa zaidi ya asilimia 90. Armadillo pia hula mimea, minyoo na mchwa.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Uzazi wa Armadillo huanza mwanzoni mwa msimu wa joto. Armadillo hubeba mimba inayodumu kwa miezi miwili hadi mitatu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Armadillo huchukua miezi 4 kurutubisha yai kabla ya kuzaa. Yai lililorutubishwa hugawanyika katika hatua nne za ukuaji wa mimba na kutoa mapacha wanne.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Watoto wa Armadillo huanza kujitegemea kuanzia miezi 6 hadi 12 baada ya kuzaliwa. Kwa kawaida Armadillo huzaa mtoto mmoja hadi 12 kwa uzao mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mambo 6 usiyoyajua kuhusu armadillo

Armadillo wana uwezo wa kuchimba ardhini, hasa maeneo yenye udongo wa kichanga na wadudu wengi ili kujipatia chakula pamoja na sehemu ya kulala.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Armadillo wana uwezo wa kubeba bakteria wanaoambukiza ukoma kwa wanadamu (Mycobacterium leprae). Hata hivyo, si rahisi binadamu kupata maambukizi ya ukoma kutoka kwa Armadillo. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu hawezi kuambukizwa ukoma na Armadillo isipokuwa kwa kumhudumia mnyama huyo mara kwa mara.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Miili ya Armadillo imefunikwa kwa gamba gumu ambalo huwasaidia kujikinga dhidi ya mashambulizi ya wanyama wakali.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Back
Top Bottom