Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wanyama hawa hutumia muda wao mwingi kulala na hutafuta chakula wakati wa asubuhi na jioni. Kwa kawaida Armadillo hulala kwa saa 16 kila siku ndani ya mashimo yao.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wakati wa uzazi na msimu wa baridi Armadillo hukusanyika katika vikundi ndani ya mashimo yao ili kupata joto jingi mwilini.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa mujibu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uhifadhi wa Asili (IUCN), wanyama aina ya Armadillo hawapo hatarini kutoweka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Paris St-Germain wanamnyatia kipa wa Manchester United na Uhispania David de Gea, 30, na huenda wakamnunua msimu huu wa joto. (Sun)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Liverpool itamenyana na Real Madrid katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 22, ikiwa mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 28, ataondoka klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England. (AS - in Spanish)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Afisa mkuu mtendaji wa Borussia Dortmund Hans-Joachim Watzke hata hivyo amesema hatarajii kupokea ofa kubwa msimu huu kumhusu Haaland au winga wa England Jadon Sancho. (Goal)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkufunzi wa Bayern Munich Hansi Flick amesema kuna ''uwezekano mkubwa'' wa klabu hiyo kumnunua mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 20. (Mail)
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okapi ni kati ya wanyama wenye kwato zilizogawanyika kati kama ilivyo kwa mbuzi, kondoo na kadhalika. Mnyama huyu anapatikana katika Bara la Afrika tu katika Nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo huko Kaskazini Mashariki katika misitu wa mvua.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wataalamu wa elimu ya viumbe husema kuwa okapi na twiga ndiyo pekee waliobakia katika kundi la Girrafidae
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okapi, kimuonekano, ana miraba kama ya pundamilia lakini kinasaba yupo karibu zaidi na twiga. Rangi yake ni kahawia na wengine ni wekundu wa kahawia.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Urefu wa okapi ni mita moja na nusu, wakati Uzito wake ni kilogramu 200 hadi 350. Okapi amejaaliwa kuwa na shingo ndefu na kichwani kwake, kwa dume, ana pembe kama zile za twiga. Badala yake, majike ya Okapi yana manyoya laini kichwani. Okapi ana masikio makubwa, yaliyosimama na yanayokamata sauti kirahisi na hivyo kumsaidia kuepuka hatari.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okapi si wanyama wanaoishi kijamaa bali ingawa mara kadhaa huonekana wakiwa pamoja katika vikundi vidogo wakiwa wanakula na hata kucheza.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chakula na uzazi
Okapi hula majani ya miti, nyasi na matunda Yeye kitaalamu huitwa ‘herbivorous’ (wanyama walao mimea tu). Okapi hutafuta riziki mchana na jioni na hupumzika zaidi usiku.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kwa upande wa uzazi, okapi hubeba mimba kwa siku 440 hadi 450, kisha huzaa mtoto mmoja. Kitoto cha okapi huanza kunyonya mara tu baada ya kuzaliwa hadi anapofikisha miezi mitatu.
 
Baada ya miezi mitatu, okapi huanza kula majani huku akiendelea pia kunyonya. Baada ya miezi sita, okapi huacha kabisa kunyonya.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mambo 7 usiyoyajua kuhusu okapi
Kama vile ilivyo kwa twiga na ng’ombe, okapi ana matumbo manne ambayo husaidia kumeng’enya majani magumu aliyoyala.
 
Okapi ana ulimi mrefu, mweusi ambao unaweza kumsaidia kuvuta majani kwenye matawi akiwa mbali.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okapi wana tabia ya kutenga maeneo yao kwa kutumia kwato zao ambazo huacha alama nene inayoonekana wazi. Madume hutumia mkojo kuweka alama zao.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ndama wa okapi ana uwezo wa kutembea dakika 30 tu baada ya kuzaliwa lakini hawezi kujisaidia, siyo haja kubwa wala ndogo, mpaka afikishe umri wa mwezi mmoja.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Wataalamu wanasema kuwa Okapi anawasiliana na mwanawe kwa kutengeneza sauti (infrasound) mfano wa kelele ambazo haziwezi kusikika kwa sikio la mwanadamu.
 
Back
Top Bottom