Armadillo hupendelea kuishi katika maeneo yenye joto na unyevunyevu. Wanyama hawa wanajulikana kwa miili yao midogo yenye rangi ya hudhurungi (zambarau) na mkia mrefu na mgumu, kichwa kirefu, macho madogo meusi, masikio marefu yaliyoelekea juu na miguu minne; miwili mbele na miwili nyuma.
Wanyama hawa wanasifika kwa tabia yao ya kuchimba mashimo kwa kutumia kucha za miguu yao ya mbele na kisha kuingia ndani yake ili kujilinda na wanyama wakali.
Kwa mujibu wa wataalamu wa elimu ya viumbe, kuna takriban aina 20 za Armadillo na aina zote hizo zinapatikana katika nchi za Amerika ya Kusini na Kaskazini.
Katika chakula, Armadillo hula wadudu jamii ya amfibia au reptilia kama konokono na funza kwa zaidi ya asilimia 90. Armadillo pia hula mimea, minyoo na mchwa.
Armadillo huchukua miezi 4 kurutubisha yai kabla ya kuzaa. Yai lililorutubishwa hugawanyika katika hatua nne za ukuaji wa mimba na kutoa mapacha wanne.
Armadillo wana uwezo wa kubeba bakteria wanaoambukiza ukoma kwa wanadamu (Mycobacterium leprae). Hata hivyo, si rahisi binadamu kupata maambukizi ya ukoma kutoka kwa Armadillo. Wanasayansi wanaamini kuwa mtu hawezi kuambukizwa ukoma na Armadillo isipokuwa kwa kumhudumia mnyama huyo mara kwa mara.