Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Siku ya Wanawake Kimataifa (International women's day) ilianzishwa mwaka 1911, ambapo tukio la kwanza la kimataifa lililotambulisha Siku ya Wanawake Duniani lilianzishwa na kikundi cha kupigania haki za wanawake.
 
Mara ya kwanza Siku ya Wanawake (Women's day) ilikua ikifanyika Machi 19. Tarehe rasmi ya Machi 8, ilitokana na siku ya likizo ya kitaifa ya Urusi kukumbuka siku ambayo wanawake walipata uhuru wa haki ya kuweza kupiga kura mwaka 1917. NB: Mojawapo ya lengo la kusherehekea siku ya Wanawake Duniani (International women's day), ni kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika maendeleo ya kiuchumi, kihistoria, kijamii n.k duniani.
 
Matukio ya ajabu hayajawahi kuisha hapa duniani. Mwaka 2015, bwana mmoja kwa jina la Joel Vazquez Rojas ambaye alikuwa ni Meya wa mji wa San Pedro Huamelula, Mexico, alifanya sherehe kubwa ya ndoa kumuoa Mamba.Mamba huyo kike alikuwa na umri wa miaka mitatu aliyepewa jina la Maria Isabela. Katika mji huu jambo hili halikua la kushangaza sana kwasababu huo ndio ulikua utamaduni wao kwa kiongozi kuoa kiumbe na kuishi nae. Utamaduni huu unaaminika kuwa ndio unasaidia kupatikana kwa samaki wengi katika pwani ya bahari ya mji huo na ikiwa hakuna ndoa kama hiyo itakayofungwa baina ya kiongozi wa mji huo na kiumbe wa namna hio, basi shughuli hiyo tegemezi kwa uchumi wa watu wa mji huo itakua ngumu. Utamaduni huu umekuwa ukitekelezwa tangu mwaka 1789 na imekua ikifanyika kila mwaka.
 
The Bunyadi ni mgahawa wa chakula uliokuwepo huko London Uingereza, ulianzishwa mwaka 2016. Baada ya miezi miwili tu ukafungwa kutokana na kuzidiwa na wateja, watu walikuwa ni wengi sana. Banyadi ni neno la kihindi lenye maana ya asili. Kila mteja anaeingia kwenye mgahawa huu anatakiwa kuwa uchi wa mnyama kama alivyozaliwa. Ukiwa ndani ya mgahawa huu ni marufuku kuwa na simu na pia ni marufuku kupiga picha. Mmiliki wa mgahawa huu Sebastian Lyall alisema kuwa siku chache baada ya kuufungua mgahawa huu zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamesha weka oda ya kula hapo, na baada ya kufungwa kulikua na oda za watu 46,000 zimebaki kupata chakula hapo, taarifa zinasema kwamba walifunga ili kutanua zaidi mgahawa huo kwakua ulionekana kuzidiwa na idadi ya watu. Mteja akishafika mgahawani hapo anaelekezwa na walinzi katika chumba maalumu ambako anaenda kuvua nguo zake alafu anarudi kuagiza chakula. Bei ya chakula ilikuwa inafika hadi Tsh 200,000=
 
Mwaka 2015, bendi ya Peking Duk waliripoti kuhusu shabiki wa bendi yao ya Peking Duk ya huko Australia, bwana David Spargo, aliefanikiwa kwenda nyuma ya jukwaa (backstage wanapokaa wasanii) kwenye moja ya matamasha yao kwa kutumia ujanja wa kujiorodhesha kama mwanafamilia kwenye ukurasa wao wa Wikipedia na kuwaonyesha walinzi wakamuamini. Washiriki wa bendi hiyo walivutiwa sana na mbinu yake walimwita na kujumuika nae kwa kupiga stori na kunywa bia pamoja naye.
 
Mwaka 1932-1933 lilitokea janga la njaa hatari sana lililoikumba Ukraine, Janga ilo liliitwa Holodomor. Kukosekana kwa chakula kulipelekea watu kuanza kulana nyama wenyewe kwa wenyewe, watu walikufa kama kuku. Watu wengine walikua wakifanya uharifu makusudi na kujipeleka Jela wenyewe wakiamini wakiwa huko Serikali itawahudumia chakula bure, hali iliyosababisha magereza yote kujaa. Janga hili la kutisha lilidumu kwa msimu mmoja tu wa mwaka 1932-33 lakini lilisababisha vifo vya watu zaidi milioni 12 katika nchi ya Ukraine. Sababu kuu za kutokea kwa janga hili la njaa ni ukame pamoja na mazao kushanbuliwa na wadudu (nzige) shambani. Kila ifikapo mwisho ya mwezi November ya kila mwaka huwa ni siku ya kumbukumbu ya janga hili nchini Ukraine.
 
Mshairi mashuhuri wa Marekani, Maya Angelou, aliahidi kumsaidia Dr Martin Luther King Jr. kukusanya pesa kwa ajili ya maandamano ya watu masikini. Sharti lake pekee ilikuwa kwamba angeenda kuifanya kazi hiyo baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa na marafiki zake. Lakini ilipofika siku ya kuzaliwa kwake, Aprili 4, 1968, Luther King aliuawa. Baada ya hapo, alikataa kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa miaka. Na kwa zaidi ya miaka 30, yeye na aliyekua mke wa Luther King, Coretta Scott King walikua wanakutana, kupigiana simu au kupelekeana maua kila Aprili 4.
 
Mwaka 1952, moshi mkubwa wa manjano ulitanda katika jiji la London kwa siku tano mfululizo na kuua zaidi ya watu 4000. Moshi huo ulitanda sana kiasi kwamba watu barabarani hawakuweza hata kuona miguu yao wenyewe walipokua wakitembea. Baadhi ya watu waliokufa hawakupata shida yoyote ya mapafu; walikufa kwa kuanguka na kuzama katika Mto Thames kwakua hawakuweza kuona mto walipokua wanatembea.
 
Miaka ya nyuma kabla ya ugunduzi wa ufutio (eraser) watu walikua wanatumia mkate kama ufutio kufuta alama za penseli. Mnamo mwaka 1770, Edward Naine kwa bahati mbaya alichukua kipande cha mpira badala ya mkate na kufutia, akaona mpira unafuta vizuri sana, hii ikamfanya aanze kuuza vifutio vya mpira
 
Huko Ohio, Marekani, mwaka 2016 Polisi waliripoti wametumiwa picha na muhalifu waliyekuwa wanamtafuta. Jamaa anaitwa Donald Pugh (pichani), aliwatumia picha Polisi na kuwaomba wabadilishe picha waliyokuwa wameweka kwenye bango la tangazo la kutafutwa kwake kwasababu ilikua inaonekana vibaya, hivyo aliwatumia picha hiyo nzuri ili watu wasimuone kama ana sura mbaya. Polisi walikubali ombi lake wakaweka picha aliyokua anataka na pia wakamshukuru kwa ushirikiano alioonesha na kumuomba kama ikiwezekana aende kituo cha Polisi wazungumze.
 
Gustaf Håkansson alipata jina la utani la 'Steel Grandpa' (Babu wa chuma) baada ya kushinda mbio za baiskeli za maili 1000 huko Sweden mnamo 1951, akiwa na umri wa miaka 66. Ingawa kwenye mashindano hayo alikataliwa kuingia kwa sababu ya umri wake, ila alijiunga kama muendesha baiskeli wa kawaida tu ambaye ashindani lakini alifikia mstari wa kumalizia mbio muda mrefu kabla ya wengine wote.
 
Baada ya Rais wa 35 wa Marekani John F. Kennedy kuuawa, mkewe Jacqueline Kennedy alikataa kuvua suti ya rangi ya waridi (pink) aliyovaa wakati mumewe anauawa. Ilikuwa imechafuliwa na damu ya John F. Kennedy aliposhambuliwa. Alivaa hata wakati Lyndon B. Johnson anaapishwa kuwa Rais wa 36 wa Marekani. Jacqueline alisema, "Nataka waone kile walichomfanyia mume wangu."
 
Mwaka 1829 Mexico ilifuta na kukataza biashara ya watumwa. Watumwa wakawa wanatoroka sehemu Mbalimbali na kukimbilia Mexico. Watu waliokua wanamiliki watumwa huko Marekani waligundua kuwa watumwa wao walikuwa wanakimbilia Mexico. Marekani ikajaribu kuifanya Mexico isaini mkataba wa watumwa waliotoroka Marekani kwenda Mexico warudishwe Marekani, lakini Mexico ilikataa kutia saini mkataba huo, ikasisitiza kwamba watumwa wote watakua huru mara tu wanapotia miguu katika ardhi ya Mexico.
 
Wakati Marcelo Bielsa alipoanza kuwa Kocha wa Leeds United, aligundua kuwa shabiki wa kawaida lazima afanye kazi masaa 3 ili kupata pesa ya kulipia tiketi ya mechi. Kwa hiyo siku moja aliwaita wachezaji wake wote pamoja na kuwaambia kuwa waokote takataka katika uwanja wa mazoezi kwa masaa matatu. Alifanya ivo kwasababu alitaka wajifunze kufahamu jinsi mashabiki wanavyofanya kazi kutimiza mapenzi yao kwa timu hiyo.
 
Ana di Pištonja, au Baba Anujka, alikuwa muuaji hatari huko Yugoslavia, ambaye alifanya mauaji kati ya 50-150 kupitia "dawa za mapenzi" ambazo aliwauzia wanawake waliokua na shida katika ndoa zao. Wanawake walipewa dawa hizi, zilizochanganywa na sumu bila wao kujua na kwenda kuwapa waume zao, ambao walifariki siku nane baada ya kutumia dawa izo. Alikamatwa mwaka 1928 akiwa na umri wa miaka 90 lakini aliachiliwa baada ya miaka nane kwa sababu ya uzee
 
Kuna ile imani kwamba ni vibaya kumuangalizisha mtoto kwenye kioo. Kama umeshawahi kusikia kuhusu imani ya namna hii tafadhali ebu tueleze kwa ufupi ni KWANINI sio vizuri mtoto kujiangalia kwenye kioo?? na pia kuna ATHARI gani? Kwa upande wangu nilisikia kwamba sio vizuri kwasababu mtoto anaweza kuota ndoto mbaya akilala.. Wewe je! kwa upande wako unafahamu nini?
 
Agha Mohammed Khan alikua muanzilishi wa Qajar dynasty huko Iran. Usiku mmoja wakati wamepiga kambi nje ya ngome ya Shushi, Agha Mohammad Khan aliletewa tikiti, alikula nusu alipomaliza, akaamuru ile nusu nyingine ihifadhiwe atakula kesho. Watumishi wake watatu wakala ile nusu iliyobaki, kesho yake wakati Agha Mohammad Khan alipotaka aletewe ile nusu iliyobaki, ilibidi wamuambie kwamba imeliwa. Alikasirishwa sana na tabia ile, akaamuru wauawe. Kwa kuwa siku hiyo ilikuwa Ijumaa (Siku Takatifu katika Uislamu), aliamuru kunyongwa kwao kuahirishwe hadi siku inayofuata na kuwaamuru warudi katika majukumu yao. Kwakuwa watumishi hao walikua wanajua kwamba Agha Mohammad Khan hashindwi kutimiza ahadi zake, haswa katika kuua mtu, waliamua kumuua kabla hajawaua! Waliingia ndani ya hema lake wakati amelala na kumchoma kisu kifuani akafa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…