Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nguvu hizo za umeme za samaki huyo aina ya Electric eel zinatajwa kuwa kwenye misuli na seli za mwili wake na mara nyingi nguvu hiyo ya umeme huitumia kwajili ya kujihami na maadui na hutumia wakati akitafuta chakula ambapo hutumia nguvu hiyo ya umeme kwajili ya kuwaua viumbe wakiwemo samaki wa kawaida kwajili ya kitoweo.
 
Maajabu ni kuwa samaki aina ya Electric eel anayepatikana katika mto amazoni kusini mwa bara la Amerika mwenye nguvu ya umeme inayofikia volt 500 na samaki aina ya Electric catfish anayepatikana katika mto Nile nchini Misri katika bara la Afrika mwenye nguvu ya umeme inayofikia volt 350 ndiyo samaki wanaotajwa kuwa na uwezo wa kumuua hata binadamu au mnyama kama tembo
 
BERMUDA TRIANGLE jina lililopewa na Vincent H Caddis mwaka 1974,kutokana na maajabu yake eneo hilo pia huitwa DEVIL TRIANGLE ( Pembe tatu ya kishetani) eneo hili linapatikana katika bahari ya Atlantiki pia ni eneo linalotenganisha maeneo matatu kwanza kisiwa cha Bermuda, mji wa Miami Florida na nchi ya puertorico, eneo hilo lina ukubwa wa maili 500000.
 
Eneo hilo linahusishwa kua na viumbe Aliens kua ndio wanaofanya matukio ya ajabu ikiwemo katika kumbukumbu zilizopo mwaka 1948 ndege aina ya NC16002 iliyopakia abiria watatu ilipotea katika eneo hilo ilipokuwa ikitoka puertoerico kuelekea miami, Frorida nchini Marekani pia miaka mitatu nyuma mwaka wa 1945 ndege 5 za kijeshi za Mrekani zilipotea katika eneo hilo la pembetatu ya shetani
 
Swali je ni kweli Aliens hupoteza Meli na ndege Katika BAHALI ya shetani??📝📝

👉katika uchunguzi uliofanywa hivi karibuni na kituo kikubwa ulimwenguni cha uchunguzi wa anga NASA, inahisiwa kuwa eneo hilo limezungukwa na nguvu za usumaku zinazofanya kutokea kwa nguvu kubwa ya uvutano inayovuta kitu chochote kinachopatikana eneo hilo au katika anga la eneo hilo la BAHALI YA SHETANI.
 
Je wajua : ndege aina ya humming ndioe ndege pekee duniani mwenye uwezo wa kuruka kinyumemnyume yani akiwa ametanguliza mkia mbele na moyo wake hudunda mara 1000 kwa dakika wakati binadamu moyo hudunda mara 70 kwa dadkika.
 
Je wajua: vita iliyopiganwa mwaka 1859 kati ya Uingereza na Marekani iliyoitwa the pig war au vita ya nguruwe ilisababishwa tu na mmarekani mmoja aliepiga risasi nguruwe wa muairishi mmoja wa uingereza kisa nguruwe huyo amekula viazi shambani mwake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…