Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kulingana na utafiti matumizi ya soda na dawa za kulevya kama kokeini (crack cocaine) husababisha kuharibika kwa meno. Asidi iliyopo kwenye soda na dawa za kulevya hushambulia ganda la nje la jino na kusababisha athari kama kutoboka.
 
Watafiti wanadai mahusiano mazuri pamoja na jamii inayokuzunguka hasa ndugu ni muhimu sana kwa kurefusha maisha kama ilivyo muhimu kwa mtu aliyezidi uzito kupunguza uzito au yule asiyefanya mazoezi kufanya mazoezi
 
Mwanamke kufika kileleni huongeza kasi ya mbegu ya kiume yenye "Y" kukutana na yai ili kufanya mimba ya mtoto wa kiume pia hupunguza kiwango cha asidi/tindikali ambayo inaweza kuua kromosomu ya "Y" kwenye mbegu za kiume
 
Kuna baadhi ya kero sugu kwenye jamii zetu ambazo zinasababisha wanawake kuhangaika sana kuliko wanaume mfano tatizo la maji, wanawake wanapaswa kushiriki kikamilifu kwenye maamuzi hasa yanayowagusa moja kwa moja.
 
Kutembea walau dakika 30 kila siku husaidia kuimarisha moyo, misuli na mifupa. Pia hupunguza mafuta mwilini na kupunguza hatari ya kuugua kisukari, maradhi ya moyo na saratani.
 
Tafiti zimedai kizazi cha sasa kinafanya tendo la ndoa mara chache zaidi ikilinganishwa na vizazi vilivyopita. Baadhi ya matatizo yanayosababisha hali hiyo ni mkazo (stress), sonona (depression), uchovu, kuwahi kufika kileleni n.k
 
Maji ya bahari yana madini mengi muhimu kwa mwili kama sodiam, kloridi, salfeti, magnesi na kalisi hivyo kuogelea baharini husaidia kuponya baadhi ya maradhi ya ngozi kama psoriasis
 
Ili kuepuka mkazo (stress) madaktari wanapendekeza ulaji chakula bora kiafya hasa matunda na mboga za majani husaidia sana. Pia, wanashauri kuushughulisha mwili kwa mazoezi na kusinzia angalau masaa 8 kila usiku
 
Katika nchi zilizoendelea watumiaji baiskeli wengi ni watu wenye pesa, maisha mazuri na elimu ya juu. Zaidi ya asilimia 70 ya wakazi wa nchi ya Uholanzi, hutumia baiskeli kwenda katika shughuli zao za kila siku
 
Watoto wa miezi 4 hadi 12 wanapaswa kulala hadi masaa 16. Watoto wa mwaka 1 hadi miaka 2 wanapaswa kulala kati ya masaa 11-14. Watoto wa mika 3 hadi 5 wanapaswa kulala masaa 10-13. Watoto wa miaka 6 hadi 12 wanapaswa kulala masaa 9-12. Vijana ni masaa 8-10. Na kwa watu wazima ni masaa 7-8.
 
Karoti zina ziada kubwa ya vitamini A, B & K na madini pengine kuliko tunda lolote lile hivyo jitahidi kujumuisha karoti kama kiungo kwenye chakula au unaweza kuitafuna ikiwa mbichi!
 
Shirika la Afya Duniani (WHO) imetaja kutembea na kuendesha baiskeli kama njia rahisi na madhubuti katika kuzuia magonjwa sugu yasiyoambukiza kama maradhi ya moyo, kupanda kwa shinikizo la damu, kisukari, saratani n.k
 
Tikitimaji linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri hivyo kupunguza hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu.
 
Kuwa kwenye mahusiano thabiti husaidia kuchochea furaha maishani kulingana na tafiti nyingi. Kuwa katika mahusiano mazuri hufanya kiwango cha homoni ya upendo (oxytocin) huongezeka sana na kuchochea ukaribu na faraja.
 
Unaweza kuhisi ngozi sio sehemu ya muhimu katika kinga ya binadamu lakini ukweli ni kwamba ngozi ni sehemu ya muhimu sana kwa mwili wa binadamu. Kwa kinga kamili ya mwili wa binadamu tunahitaji vitamini A ambayo hupatikana kwa wingi kwenye viazi vitamu.
 
Kuendesha baiskeli kwa saa 1 kila siku kwa siku 7, hukusaidia kuchoma nusu kilo ya mafuta kutoka katika mwili wako. Mwendesha baiskeli ana moyo imara unaofanya kazi kwa ufanisi, kuliko mtumiaji wa gari au pikipiki
 
Mapera husaidia kuweka uwiano sahihi wa madini ya sodiamu na potasiamu kwa mwili wako hivyo kuweka sawa shinikizo la damu. Pia hupunguza kiwango cha lehemu (cholesterol) na kuepusha maradhi ya moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…