Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Shida ni ile ile hata kwenye hii chanjo ya Johnson and Johnson. Damu inaganda kwenye ubongo na waathirika wakuu ni wanawake ambao hawajafikia menopause. Na matibabu yake kuondoa hiyo damu iliyoganda ni tata. Matibabu ya kawaida ya kutumia clot bursting drugs hayafai...

Guinea pigs...mamilioni kwa mamilioni ya watu...
View attachment 1752105
Duh....mbona hatari
 
FB_IMG_1618417850412.jpg
 
Muwe na Wakati mwema

Barabarani, unakutana na mwanamke mchuuzi masikini mwenye mtoto mgongoni, unashusha kioo cha gari lako na kumuuliza kwa sauti ya kijeshi:

"Unauza bei gani hivyo vitunguu na hizo ndizi?" Muuzaji masikini kwa upole anakujibu "shilingi elfu moja kwa kichane cha ndizi, na elfu moja kwa fungu la vitunguu." Kwa kiburi unamwambia unahitaji kichane cha ndizi kwa shilingi mia tano na fungu la vitunguu kwa shilingi mia tano, au vinginevyo haununui.

Muuzaji masikini anakubaliana na hali na kukujibu, "Chukua tu kwa bei unayotaka, sijauza chochote tangu asubuhi, walau sasa nipate cha kununulia watoto chakula cha usiku."

Amepata hasara, lakini zaidi anaenda kukununulia pia mfuko wa kuweka bidhaa hizi ulizo nunua. Unamwagiza afanye haraka vinginevyo utabadili mawazo. Anaomba msamaha, na kwa tabasamu anakukabidhi bidhaa zako, anakubariki pia kwa kumuungisha.

Unamrushia hela na kuchomoka kwa kasi na kumwachia wingu la vumbi na moshi linalomfunika yeye na mtoto. Anakohoa wakati anaweka vizuri fedha kidogo alizopata. Umaskini haujamwachia uchaguzi.

Umefika sasa kwenye hoteli ya nyota tano, ambapo utakutana na rafiki zako. Unawaambia waagize chakula na vinywaji kadiri wanavyotaka. Wanaagiza vyakula vya gharama kubwa, na mabaki ya chakula ni mengi kuliko chakula walichokula. Gharama nzima inakua shilingi laki tano. Unalipa bila kuomba upunguziwe, unampa mhudumu tip ya shiligi elfu kumi shukrani kwa chakula alichowahudumia ambacho hamkula hata nusu yake.

Tukio hili linaweza kuonekana la kawaida kabisa kwako, lakini sio la kibinadamu.

Point ni kwamba:-
Kwanini kila mara tunaonyesha tuna nguvu ya kubishania bei wakati tunaponunua kutoka kwa maskini?
Kwanini tunakua wakorofi tunaponunua kwa maskini?
Kwanini tunakua wachoyo tunaponunua kwa wahitaji?

Kwanini tunaonyesha ukarimu kwa wale ambao wala hawahitaji ukarimu wetu?
Kwanini tunaonyesha upole na utu tunaponunua kwa watu matajiri ambao wanaona hela yetu kama chenchi ndogo tu?
Kwanini tunaelekeza fedha zetu kwenye bahari ya fedha?

#Tafadhali nunua vitu rahisi kwa watu mskini kwa bei ya haki

#Wakati mwingine, makusudi lipa na ziada unaponunua kutoka kwa mwanamke masikni.

NIMEISOMA MAHALI NIKATAFSIRI.*Wakati mwema
Ukumbusho huu unawahusu watu ambao Mwenyezi Mungu amewajaalia Imani kwenye kifua vyao.
Walevi, wazinzi na wahuni hili wala hawajali
 
Back
Top Bottom