D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,665
- 121,102
Hata hivyo, kama nilivyosema kuwa wakati mwengine kulikuwa na mambo yanatugonganisha katikati ya umoja huo. Mojawapo ni la mpira wa miguu, hasa baina ya sisi wa Mchangani na hao wa Pandani ‘wenyewe’. Timu yetu ilikuwa ikiitwa Mchangani Stars na ya Pandani ikiitwa OPEC. Yetu ilikuwa chini ya udhamini wa Hamad Shamata na aliyekuja kuwa Shemegi yake, Muhsin Khamis Melek. Nadhani OPEC ilikuwa chini ya udhamini wa akina Humoud Al Maamiry na ilikuwa ikipata sana vifaa kutoka jamaa zao wa nje, hasa Arabuni. Basi baina ya timu hizi mbili, uhasama wake ulikuwa wa ajabu.