Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

1618520920560.png
 
Huo huo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Liugali linaterezaga tu.
Baba mkwe alinisihi nisikose kula hiyo, ina umuhimu sana mwilini.... Umuhimu wenyewe hakuniambia.
Nikawaza kiutu uzima tu kuwa labda una nanihii nanihii
Ushindweeee!!! [emoji16][emoji16][emoji16]

Halafu hata mahari hujamalizia. Roho inaniuma miye [emoji24][emoji24]
 
kwetu sisi Ijumaa ni siku maalum kwa viongozi wakuu kutoa nasaha zao kwa wananchi

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanyonge wakiwemo wajane, mayatima na mafakiri.

Alhaj Dk Mwinyi aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akiwasalimia Waumini wa dini ya Kiislamu huko katika Masjid Tawba maarufu Jongeyani uliopo Malindi kwa Tausi, Wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi mara baada ya kumaliza Sala ya Ijumaa.
1618521124259.png
 
Katika salamu zake hizo, Alhaj Dk. Mwinyi alisema kwamba kila mmoja kwa nafasi yake ni vyema akaona haja ya kuyasaidia makundi hayo katika jamii ili na wao waweze kuitekeleza ibada ya funga ya Ramadhani ipasavyo.

Pia, Alhaj Dk. Mwinyi alitoa wito kwa wafanyabiashara wote kwamba mwezi mtukufu wa Ramadhani ni mwezi wa kuhurumiana hivyo, mfanyabiashara anatakiwa kupata faida ya kiasi na sio kupata faida mara mbili kwani hilo si jambo la busara.

Kutokana na hilo, Rais Dk. Mwinyi aliitaka Taasisi za Serikali zenye kushughulika na kuhakikisha kwamba bei elekezi zinafuatwa wafanye wajibu wao kuzuia wimbi la wafanyabiashara kupandisha bei mara kadhaa katika kipindi hichi cha mwezi wa Ramadhani.
1618521199306.png
 
Back
Top Bottom