Kilichokuwa muhimu ni kuwa hata wakati huo nikiwa mdogo, tayari Maalim Seif alishakuwa alama ya nguvu ambayo nadhani sikuwa peke yangu niliyeijuwa, kuihisi na kuihusudu. Nguvu hii ikisafirishwa kwa matukio na simulizi za mikasa, hasa ile ya kupimana nguvu kati yake, Maalim Seif, na Mwalimu Julius Nyerere
Mkasa mmoja tukiambiwa Mwalimu Nyerere alikuwa akimualika Maalim Seif akamtembelee mama yake Butiama, naye Maalim Seif akamuambia angelikwenda baada ya yeye Nyerere kurudi kumuona mama yake, Maalim Seif, Bi Time, huko kwao Mtambwe.