Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Takwimu za Kikabila Zanzibar
Ukiiweka kando propaganda inayolinganisha Ubantu peke yake na Uafrika utakuta Marais wakubwa wa Kiarabu wa Kaskazini ya Afrika, marehemu Gamal Abdel Nasser, na Ahmed Ben Bella ambaye yuhai, walikuwa upande wa ASP na TANU katika kuyafanikisha mapinduzi ambayo kijuujuu yamekuwa yamefahamishwa na kufahamika kuwa yalikuwa mapinduzi ya “Waafrika” wanyonge dhidi ya “Waarabu” mabepari wa Zanzibar. Kana kwamba hao Waarabu wote wa Zanzibar walikuwa matajiri na mabepari.
 
Akitumiya takwimu za Michael Lofchie, Profesa Issa G. Shivji ameeleza yakuwa asilimia moja (1) tu ya jamii ya Kiarabu ilokuwa ikiishi Zanzibar kabla ya Mapinduzi ilikuwa katika tabaka la juu la kijamii, na asilimia 76 ya Waarabu walikuwa katika tabaka la chini. Kwa mujibu wa takwimu za kikabila za 1948 Waafrika Asilia (Washirazi) walikuwa asilimia 56.2, Waafrika kutoka bara walikuwa na asilimia 19.4, Waarabu asilimia 16.9, Wahindi asilimia 5.8, na Wangazija asilimia 1.2
 
Na hao hao Waarabu wa kawaida wa Kizanzibari waliokuwa wakulima, wavunjaji mbata na wazegazega hubebeshwa tuhuma za utumwa. Na katika hiyo asilimia 1 ya tabaka la juu na la kati la Kiarabu ipo haja pia ya kujiuliza Waarabu wa Zanzibar wakijiona kama raia au watawala? Kama watawala mbona hawajazijaza skuli za Kiarabu nchini? Mbona wengi wao walikuwa hawaijuwi lugha ya Kiarabu? Na nini mchango wa Waarabu katika kuijenga Zanzibar?
 
Leo Mji Mkongwe wa Zanzibar una heshima ya Kimataifa (World Heritage Site) uliopewa na shirika la UNESCO la Umoja wa Mataifa (UN). Wakfu wa mwanzo wa maji ya mji wa Zanzibar ulianzishwa na Sayyid Barghash bin Said bin Sultan. Mchango wa Wahindi hauelezwi vya kutosha na khasa katika kuigharimiya misafara ya utumwa, au kuipa misaada ya kifedha chama cha AfroShirazi, au hata mchango katika kazi za udobi, ukataji nywele, au kuuza vifuu.

Na huenda sababu ikawa kutaka kuonyesha pengo la kibaguzi baina ya Waafrika kutoka bara (asilimia 19.4) na Waarabu (asilimia 16.9). Takwimu hazisemi asilimia ngapi kati ya Waafrika kutoka Bara na Waarabu walikuwa Wazanzibari kisheria au kinyume na sheria.

mwisho wa sura ya pili
================================================
 

Attachments

Hahahahahaha sikujua kama kwenye huu uzi kuna mapimbi [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna mtu na pimbi wake[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ila wote kwa muda mrefu wamepotea.
Huu uzi pia una malkia mchawi anaitwa ISISI mke wa Mzee wa liver[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hapa pana burudani za kila aina
 
Aisee...
 
Haarua 😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…