Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jitahidi Walau Kufikia Saa Mbili Usiku Uwepo Nyumbani Chukua Biblia/vitabu vya Dini Pitia Pitia Vifungu Kadhaa Pata Chakula Cha Usiku Kisha Pumzika,Kwakufanya Hivyo Unajiepusha Na Hatarii Mbalimbali Usiku Unamambo Mengi Sanaa.
True
 
Timu za Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia zimefuzu kutoka ukanda wa Afrika kucheza fainali za kombe la dunia ziakazopigwa baadae mwaka huu huko Qatar, kufuatia matokeo yao ya michezo ya jana.
 
Cameroon ikishinda ugenini 2-1 dhidi ya Algeria kwa bao la jioni na kufuzu kwa bao la ugenini baada ya mchezo wa kwanza Algeria kushinda ugenini bao 1-0. Ghana ikaiondosha Nigeria kufuatia sare ya 1-1 ugenini, mchezo wa kwanza uliopigwa Ghana, timu hizo zilienda sare ya 0-0.
 
Morocco ikachafua sherehe ya kumkaribisha mwanachama mpya wa Jumuia ya Afrika Mashariki, DRC baada ya kuitandika 4-1 huko Casablanca na kuiondosha kwa jumla ya mabao 5-2 kufuatia mchezo wa kwanza mjini Kinshasa kwenda sare a 1-1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…