Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kulingana na ripoti ya Dr. Barry S. Kendler wa Manhattan College, kwamba utumiaji wa kanuni fulani za vitunguu saumu na/au vitunguu maji una mchango chanya katika kuzuia hatari ya kupata ugonjwa wa atherosclerotic.
 

Chromium husaidia mwili kudhibiti kiwango cha na sukari ya kwenye damu na kuhakikisha utoaji wa taratibu, kidogokidogo wa glucose kwenye misuli na seli za mwili.​

 

Zaidi, ripoti ya tafiti ya Mathew PT na Augusti KT iliyochapwa kwenye jarida la 'Indian journal of Physiology and Pharmacology', ilionekana kwamba juisi ya kitunguu, ilipopewa kwa wagonjwa wakisukari pamoja na vyakula vyao, ilisaidia kudhibiti hyperglycemia (sukari ya juu ya damu) kisawasawa.​

 

Kwahiyo basi, kula vitunguu kunaweza kusaidia kuweka sawa viwango vya sukari ya damu, ambayo ni muhimu kwa wagonjwa wa kisukari.​

 
Harufu ya kitunguu pia husababisha wadudu kukimbia, ndo maana vitunguu vinaweza kutumika kama vifukuza wadudu vilevile kutumika kutuliza maumivu ya aina fulani za kung'atwa na wadudu.
 
Tafiti zilizochapwa kwenye jarida la Utafiti wa uzuiaji wa kansa (Cancer Prevention Research) zimeonyesha kwamba utumiaji wa mbogamboga kama vitunguu saumu na vitunguu maji ambavyo vinatokea kwenye kundi la Allium husaidia kuzuia magonjwa ya kansa, hasa kansa ya utumbo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…