Gelada' wanapatikana Ethiopia, kwa muonekano unaweza kufikiri wanakula nyama zaidi lakini 90% ya chakula chao ni majani. Muonekano huo wanapenda kuutumia zaidi kama kivutio na kujilinda kama ukitokea ugomvi!
Tafiti: Wanawake matajiri wana uwezekano mdogo zaidi wa kuchiti' kimapenzi kwa wenza wao tofauti na wale ambao ni masikini, Kwa Wanaume matajiri ndio wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanya hivyo
Pomboo (Dolphins), na wao hupeana majina wenyewe kama Binadamu. Wanasayansi wanasema, Pomboo wanaitana kwa kutoa sauti fulani kama mluzi ambayo kila mmoja huitikia kila anaposikia sauti fulani ambayo ni kwa ajili yake pekee.
Mamba wa mto Nile' ndio mnyama mchokozi zaidi kuliko wote Duniani. Anawekwa kua kinara yote kwa sababu ndio mnyama pekee ambae humchukulia Binadamu kama chakula cha kawaida tu 😌
Inland Taipan Snake' wanapatikana kwa wingi Australia, mng'ato wake mmoja tu ambao ni sawa na dozi moja ya sumu yake ina uwezo wa kuua zaidi ya Panya 250,000 na kama itatumika kwa binadamu ni 100 kwa wakati mmoja!
Maji mengi zaidi hutumika kutengeneza chupa ya maji kuliko hata maji ambayo huwekwa kwenye chupa. Kwa mujibu wa utafiti, ni kutengeneza chupa maji zaidi ya mara 6 - 7 hutumika kuliko maji ambayo yanawekwa kwenye chupa
Matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii mojawapo ni kuheshimu faragha za watu na maeneo husika mfano, Kwenye kambi za jeshi kupiga picha maeneo hayo huwa ni kosa kisheria kwa sababu za kiusalama zaidi hivyo ni muhimu kuzingatia taratibu hata kama lengo lako lilikua ni zuri.
Marekani ndio nchi inayoongoza kwa utoaji na usambazaji (exporting) wa mbegu za kiume (sperms) kwa wingi zaidi. Moja ya sababu ni hakuna sheria nyingi zinazobana uchangiaji wa mbegu hizo ambazo wananchi kutoka nchi nyingine mbalimbali hususani Canada huagiza kwaajili ya kufanya upandikizaji na kupata mtoto!
Tafiti: South Korea, Wanaume ndio wanaoongoza kwa kutumia vipodozi zaidi kuliko Wanawake. Moja ya sababu ni muonekano wako nchini humo unapewa nafasi kubwa zaidi, hata sehemu za kazi unaweza kunyimwa nafasi kutokana na muonekano wako!
India: Amar Bharati kwa zaidi ya miaka 45+ (tangu mwaka 1973) ameishi kwa kuinua mkono wake juu mfululizo bila kushusha. Kwa mujibu wake ameamua kufanya hivyo kama kutoa heshima kwa mungu wake 'Shiva (God from Hinduism) pia kusisitiza na kukumbusha umuhimu wa amani Duniani
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.