Kupanda: Hii ndiyo hatua ya mwanzo. Ni kama vile unapanda mbegu shambani. Unajifunza, unawekeza muda na bidii, lakini bado hakuna kitu cha kuonyesha. Wengi wanachoka hapa kwa sababu matokeo hayaonekani mara moja.
Kukuza: Hii ndiyo hatua ya kazi kubwa. Unapalilia, unamwagilia, na wakati mwingine unakutana na upepo au ukame. Hapa ndo inahitaji subira na nidhamu. Wengi hukata tamaa, lakini ukivumilia, unaanza kuona mimea ikikua.
Kuvuna: Hii ni hatua ya furaha. Unavuna matunda ya jasho lako. Lakini kumbuka, huwezi kuvuna usichokipanda, na huwezi kupanda leo na kutarajia kuvuna kesho
Kama kuna kazi ngumu kuifanya kwenye safari ya maisha haya ni kujikabili. Maumivu ya kukubali kuwa saa nyingine sisi ndio tatizo kubwa linalohitaji kushughulikia ndiyo yanayofanya kazi hii iwe ngumu kupindukia.

Ingawa mara nyingi tunafikiri watu ndio maadui zetu, hawatutakii mema, ukweli ni kwamba sisi wenyewe tunaweza kuwa maadui zetu wakubwa na kwa tabia zetu tunajihujumu wenyewe

Tukiweza kuishinda hofu ya kukikabili kivuli chetu kwa kuacha kuchukulia mrejesho hasi kama chuki, wivu na husda, na kutokuwa wepesi kuwageuzia kibao wale wanaoyaona matatizo yetu, hapo ndipo safari ya kujitambua inapoanza.

JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.