Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Dunia ni duara lakini si kila anayeishi ndani yake huishi huru. Wengine wamenaswa katikati wanazungushwa na presha, maamuzi ya wengine na mitazamo ya dunia.Wachache wamesimama nje ya duara wanazunguka duniani kwa mwelekeo wao wakitawala maisha yao..Jitahidi uwezavyo Uwe nje ya mduara na uzunguke nao
 
Maisha yana miiko, kanuni na desturi zake, ukiivunja nawe tarajia nayo ikuvunje huko mbele ya safari."
 
Watu makini wako kwa ajili ya kufidia wazembe, watu rahimu kufidia watu katili na werevu kufidia wajinga. Usilalamike, timiza wajibu wako.
 
Ukitaka kuiishi PEPO hapa duniani, watue watu mzigo si kuwatwisha, wasitiri si kuwaanika, wafariji si kuwasononesha, wafute machozi si kuwaliza
 
Usiitathimini siku yako kwa mavuno unayovuna bali kwa mbegu ambazo unapanda. Kumbuka kila siku una fursa na nafasi ya kupanda kitu kwa ajili ya kesho yako na sio kila siku utakuwa unavuna
 
Hakuna kujifunza kusiko na gharama, kama si fedha basi maumivu na makovu. Isingekuwa hivyo basi kujifunza kusingekuwa na maana wala umuhimu.
 
Hali ya maisha yetu ya kesho itategemea sana na jinsi tunavyoruhusu MATUMAINI au HOFU kutawala maisha yetu
 
Kama kweli tunaamini kwa dhati kuwa kuna maisha mapya baada ya kifo, na kama tunaamini ni matamu kuliko haya, basi tusingeogopa mauti hakika
 
Mabadiliko unayoyaasisi na unayotamani yatokee huishia kwenye ncha ya kidole chako punde unaponyooshea lawama na wajibu huo kwa mwingine
 
Ikiwa matamanio ya mabadiliko ya kila mtu yangetimia dunia isingetabirika wala kutawalika. Ndio sababu majaribio mengi huyeyukia njiani."
 
Usicheke tone la machozi la mwingine, maana kesho hujui nani ata kufutia lako. Dunia ni duara, huzunguka kwa siri za Mungu, leo una tembea juu, kesho unawezi kuwa chini, na unaye mwona dhaifu leo, ndiye atakaye kuwa msaada wako kesho
 
Majaribu hutuleta pamoja na kutukumbusha kuwa tu kitu kimoja na tunaunganishwa na tunu moja ya utu."
 
Huna Kitu Cha Kufanya ili Upendwe na Watu Wote Waliokuzunguka Hivyo Bhasi Kamwe Usiumize Roho Yako Eti Kwa Sababu ya Chuki za Baadhi ya Watu
 
Back
Top Bottom