Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati hupita, na unayoyapitia nayo yatapita. Hata kalenda hupitwa na wakati."Wanaotuvuruga, wanatupangua na kutupanga upya."
 
Ujuzi wa kujua jinsi ya kuishawishi na kuongoza akili za watu unaweza kukufanikisha na kukufanya uwe tajiri zaidi kuliko vyeti vya karatasi pekee vinavyoweza kufanya.
 
Kwenye Maisha, Usipofahamu Unapokosea, Jiandae akukosea kila siku, Na Mwishowe Utakata Tamaa Na kushindwa.
 
Harakati zote za maisha hatimaye ni kuizengea, kuipata na kuiishi furaha. Mengine yote ni ziada."
 
Chuki ni mzigo mkubwa unaomtesa aliyeubeba kushinda aliyelengwa na chuki yenyewe.Upendo ni mwepesi kwa aliyeubeba na mzito kwa aliyelengwa."
 
Huwezi KUWAZUIA binadamu KUSEMA. Wasiposema UPENUNI watasema SIRINI. KUSEMA ni KUPUMUA kwa AKILI
 
Mtazamo wetu katika maisha juu ya masuala, vitu na watu ndio hufanya jambo dogo kuwa kubwa na kubwa kuwa dogo. Mtazamo wako ni tatizo lako!
 
Maumivu ya kuumwa yanaambatana na mashaka na hofu lakini maumivu ya tiba huambatana na matumaini. Maumivu yanatofautiana
 
Heri kukosea katika kufurahi kuliko kunyong'onyea katika kupatia. Kuitafuta furaha ndio sababu ya kuishi, ukiipata ilinde kwa wivu mkubwa!"
 
Gharama ya kuwaelewa watu ni ndogo kuliko kuwaelewesha, kuwakubali ni ndogo kuliko kuwabadili na kuwasamehe ni ndogo kuliko kuwa na kinyongo
 
Maamuzi sahihi huwa wazi, lakini ujasiri wa kuyaamini ni jambo lingine.
 
Uvivu hauwezi kushinda mtu aliye na kusudi, hofu haiwezi kushinda moyo uliojaa imani, na wasiwasi hauwezi kufunika nuru ya matumaini ndani yako.
 
Back
Top Bottom