Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usikubali wakudharau sababu ya njaa na shida zako, Ipo siku utaikosa heshima Hata kipindi ambacho Utakua Umeshiba.
 
Kiburi chako kinaweza kukulaghai ukadhani labda watu wanakuhitaji wewe kumbe ni wewe ndio unahitaji watu
 
Usitafute nafasi ndani ya chumba cha fursa , Kama unaweza miliki jengo zima kisha uwapangie nani aingie nani asiingiie
 
Hakikisha Biashara yako haitegemei wateja mnaojuana kila siku pata wateja wapya sio kwa huruma zao bali kwa ubora wa bidhaaa yako
 
Usimsahau kamwe aliyekusaidia wakati wengine wote walikuwa wakitafuta sababu
 
Ukitupa jiwe kwenye kundi la mbwa wengi, Atakae bweka ujue ndio Kaumia sana.
 
Jifunze kustawi kimya kimya ukijua kuwa miti mirefu haikui haraka bali kwa uthabiti wa mizizi isiyoonekana.
 
Ua hata linachanue kiasi gani haliwezi kumvutia kila mtu hivyo kwenye maisha hata ujitoe kiasi gani huwezi pedwa na kila
Mtu
 
Usipange sana maisha yana mipango yake kwa ajili yako kumbuka hata baadhi ya nyakati nzuri maishani mwako hukuzipanga
Kabisa
 
Kuna maumivu mengine huwa hayataki dawa kabisa, Yanataka tu uondoke au wao ndio waondoke ili Ubaki na Amani ya Moyo
 
Kitendo cha kutafuta hadi kupata ni kitendo chanye mchakato mrefu sana wenye mambo mengi lkn kitendo cha kupoteza ni chenye sikunde chache mno.
 
Kwasababu wewe ulipitia magumu wakati unatafuta haina haja ya kuweka ugumu kwa wanaotafuta sasa mambo yameshakuwa mepesi kunjua tu kuna baraka ndani ya hilo pia mfundishe tu mtu nidhamu ya kazi kisha mengine muachie mwenyewe..
 
Ukiwa mahiri na jasiri na mwenye kujiamini kwa kila jambo basi jua kabisa watakuofia na pengine watatengeneza kila aina Ya ujmaa kuweza kukupoteza au kukudhoofisha kwa kile ambacho unafanya..
 
usikimbilie maisha ya haraka vitu vya thamani havijengwi kwa siku moja. Mvua ikinyesha leo, miti haikui kesho; inahitaji muda, uvumilivu na mizizi imara. Vivyo hivyo na maisha yako jenga ndani kabla nje haijaona matokeo.
 
Tumbo lenye njaa, Miguu iliyo peku, Pochi isiyo na hela, Moyo uliovunjika, Unaweza Kukufunza Vitu muhimu sana kwenye Haya Maisha.
 
Jifunze kuyatambua makosa yako,sikuhizi watu hawarekebishi watu wanasubiri ukosee wakuwambe!!
 
Watu wana mambo yao mengi kichwani, kwanini unahisi wanawaza mambo yako?
Ishi maisha yako, watu hawajali kama unavyojihisi.
 
Back
Top Bottom