Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usikubali hofu ikutawale, maana hofu inaleta unyonge, ukiikubali hofu, unakubali kushindwa mapema. Hata pale unapokosea, usijalie huzuni… bali jifunze. Kwa sababu kila kosa ni darasa, na kila darasa ni silaha ya kujenga maisha
 
Kuna moto ndani yako ambao haupaswi kuzimwa na maneno ya watu, kikwazo au kushindwa. Kila wakati unapotaka kukata tamaa, kumbuka ni kwa sababu uko karibu na hatua muhimu. Shujaa wa kweli hasimami katikati ya vita anasimama hata damu ikitiririka.
 
Wakati mwingine utajikuta kimya, si kwa sababu huna nguvu, bali kwa sababu umekomaa. Wakati wengine wanalalamika, wewe anza kufanya. Wakati wengine wanataka sifa, wewe tafuta matokeo.
 
Maisha yako yatafanana na marafiki ulio nao. Ukiwa na marafiki wavivu, utarithi uvivu wao. Ukiwa na marafiki wa hovyo, utarithi maumivu yao. Mwanangu, heshimu nafsi yako kwa kuchagua marafiki wanaokupa nguvu, si wanaokupoteza.
 
Tunasali sana Halafu Tunacheka na wale Waliotamani Kutuona Tunalia.
 
Linda amani ya moyo wako, maana ndiyo hazina kubwa kuliko mali zote
 
Katika maisha adui ambaye hajifichi kwako huwa ni mzuri sana anakufunza mambo mengi kuliko adui usiyemjua..
 
Kwenye maisha ukifikia ule umri wa kung'oa jino na Halioti tena, Basi Hakikisha Hupendi tena Magomvi.
 
Huwezi kuwa mwenye nguvu ikiwa muda wako unautumia na kila mtu, muda wako ndio nguvu zako utunze
 
Mungu akupe nguvu ya kupambana na changamoto zako na akuwezeshe kushinda leo na siku zote
 
Usimuonee huruma mtu ambaye amekusaliti, Jiulize kwa nini yeye haukona huruma kipindi anafanya Usaliti.
 
Nyangumi ni mnyama mkarimu na mstaarabu
wala hawezi kufanya uvamizi kwa binadamu,
na hata aonapo vyombo hivyo vya usafiri
huvipisha na kwenda kando, hutambua
kwamba binadamu hupenda kuwatazama basi
agunduapo vyombo hivyo pamoja na kwenda
mbali, huanza kufanya mbwembwe ili
mumuone ikiwa ni pamoja na kuogelea,
kurusha maji na kuurusha mwili wake.
 
Pamoja
kwamba ni mla nyama lakini hali binadamu!
Ukiwa kwenye meli akajirusha unaweza
kuzimia kwa presha kumbe wala kiumbe wa
watu hana hata shida na wewe na anataka
ufurahi kumuona.
 
Kwa ukubwa wake, binadamu wameweza
kutengeneza hata hadithi ya kwamba anaweza
kutengeneza kisiwa na binadamu wakafanya
shughuli zao juu ya mgongo wake mpaka hapo
atakapoondoka, ifahamike hadithi hiyo haina
ukweli kuhusiana na maisha ya mnyama huyu,
ni utunzi wa kufikirika.
 
Back
Top Bottom