Dunia ni duara lakini si kila anayeishi ndani yake huishi huru. Wengine wamenaswa katikati wanazungushwa na presha, maamuzi ya wengine na mitazamo ya dunia.Wachache wamesimama nje ya duara wanazunguka duniani kwa mwelekeo wao wakitawala maisha yao..Jitahidi uwezavyo Uwe nje ya mduara na uzunguke nao
Usiitathimini siku yako kwa mavuno unayovuna bali kwa mbegu ambazo unapanda. Kumbuka kila siku una fursa na nafasi ya kupanda kitu kwa ajili ya kesho yako na sio kila siku utakuwa unavuna
Usicheke tone la machozi la mwingine, maana kesho hujui nani ata kufutia lako. Dunia ni duara, huzunguka kwa siri za Mungu, leo una tembea juu, kesho unawezi kuwa chini, na unaye mwona dhaifu leo, ndiye atakaye kuwa msaada wako kesho