Nyati hupendelea kuishi maeneo ya misitu iliyo
pembeni mwa mito ambako maji hupatikana
kwa wingi hii ni kutokana na mahitaji yao ya
chakula na maji kwa wingi kwa ajili ya miili yao
kuwa mikubwa.
Nyati jike hubeba mimba baada ya miaka 5
toka alipozaliwa na mimba huchukua miezi 11
mpaka kuzaa na mara nyingi huzaa ndama
mmoja kila baada ya miaka miwili katika uzazi
unaoweza kutokea wakati wowote wa mwaka
hasa wakati wa mvua ambapo majani huwa ni
mengi.
Baada ya kuzaliwa ndama hulambwa na
mama yake hivyo kujijengea uhusiano wa
muda mrefu, ndama jike hukaa katika uangalizi
wa mama kwa muda mrefu kuliko madume
ambayo hufukuzwa baada ya miaka minne.
Faru Javan na Faru Indian ni jamii ya faru
wenye pembe moja tu kichwani isipokuwa faru
Sumatran pekee ndio mwenye pembe mbili
kama walivyo faru wanaopatikana bara la
Afrika.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.