Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

ambapo huwa
milion moja na nusu mpaka milion mbili,
wakitoka Tanzania kwenda nchi jilani na baada
ya hapo hugeuza tena, katika safari yao hiyo
nyumbu zaidi ya laki mbili na nusu hufa kwa
sababu ya ajali, kuuwawa na wanyama wala
nyama, njaa pamoja na magonjwa.
 
Wanyama wanaowawinda sana viumbe hawa
ni pamoja na Simba (Mfalme), Fisi (bwana
afya), Mbwa Mwitu (wazee wa heka heka)
pamoja na chui, duma (mapaka)
 
katika jamii yao nyumbu huwa wanasaidiana katika tatizo lolote lakini si kutoana kwenye midomo ya vifo,ukinaswa huko hilo ni lako,
 
kidogo majike
huonesha ubabe pale watoto wao
wanapokamatwa na hii ni kutokana na ile siri
ya uchungu wa mwana
 
hili ni moja kati ya
jambo ambalo huwafanya binadamu kusema
kwamba nyumbu ni wajinga kwakuwa wao
wanakuwa wengi lakini wanamkimbia labda
simba mmoja,
 
Hubeba mimba kwa kwa umri sawa nabinadamu miezi tisa, ingawa wengine huzaahata kwa miezi nane.
 
Jike anapozaa si lazima atulie anaweza
kuendelea na shughuli nyingine huku tendo hilo
likiendelea
 
Pembe zao ni silaha kali sana kwani
zimechongoka mno, ikikupigia ni kama kisu
kimepenya.
 
Michezo yao wawapo wawili wawili ni
pamoja na kudanganya mmoja kafa na
anayebaki atahakikisha anamuamsha
mwenzie.
 
Jamaa hawa ni wazalendo sana baina yao,huweza jirusha katika bonde kubwa ambalo ana hakika hawezi pona, lakini kwa kufanyahivyo bonde hilo litatengeneza njia kutokana nakumomonyoka kwa udongo na wanaofuata watapita hapo kwa urahisi kabisa ingawa wenzao watawaacha hapo marehemu auvilema, unapoona mchezo huo lazima uwahukumu wajinga.
 
Wanapoamua jambo lao pasina kujari
vikwazo vilivyo mbele huwa ni lazima watimize
agano lao, ndio maana huweza kuvuka mto hali
ya kuwa ndani ya maji washawaona mamba na
hapa ndio binadamu mnawasema wajinga,
lakini wao hujua wanafanya nini kuliko kundi
lote life njaa ni bora wachache waliwe na
mamba lakini watakao salimika wakapate
chakula ng'ambo ya pili.
 
Katika jamii zao ukikaa mbele ndio
umeukwaa uongozi hawapigi kura kama mbwa
mwitu.
 
Sauti watoazo huelewana kwa urahisikwamba kuna hatari au vinginevyo.
 
Hulala kwa zamu, kwa mfano wakiwa kumi
watano watalala huku watano wakiwalinda
wenzao na wanyama wakali, na muda ukienda
itakuwa zamu yao kulala na wenzao kupiga
ulinzi.
 
Nyumbu ni miongoni mwa wanyama ambao
ukimpiga picha rangi yake hutofautiana kidogo
na rangi zao, wana rangi nzuri sana ya kuvutia
tofauti na tuwaonavyo katika picha hizi
 
Muda mfupi tuu baada ya kuzaliwa mtoto wa
nyumbu huanza kutembea, na hii humsaidia
mtoto kwakuwa maisha yao ni ya kuhama
hama.
 
Nyati ni miongoni mwa wanyama watanowakubwa zaidi wanaopatikana hapa Afrika,
 
ni
mnyama asiyetabirika kwani anaweza kuwa
muoga ghafla akabadilika kuwa mkali sana
wakati anapokua hatarini au kujeruhiwa.
 
Nyati au Mbogo wanapatikana maeneo ya
Savana ni wakubwa na maumbo yenye uzito
mkubwa wanaumbo linalo fanana na ng’ombe
 
pia wanazo pembe zenye rangi yenye
kuwafanya waonekane wenye nguvu na
kutisha.
 
Back
Top Bottom