Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Pamoja na kwamba ni mnyama ambaye jina
lake linakuzwa sana kwamba anatabia ya kula
mizoga,
 
lakini fisi ni mnyama anayewinda na
hula nyama fresh, akikosa mawindo yake
hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na
inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutana
na mfupa,mzoga yeye hana neno.
 
Wakati wanyama wengine wengi wakiwa
wanaongozwa na madume, ukifika katika koo
za fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na
uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kuliko
dume,
 
bahati waliyonayo mbaya wanyama
hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike
lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati
mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa
wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa
watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada
kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
 
Fisi ni mnyama mnyonge lakini huweza kupora
chakula kwa wanyama wakali kama simba.
 
Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali
mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120
yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani
ukiwa umeanguka either kwa kuishiwa nguvu
au misuli kukaza na hapo ndio atafanya
biashara yake kwa urahisi, na sifa hii ndio watu
husema eti anasubiri mtu adondoshe mkono
wala sio kweli, ana akili zake.
 
Fisi ana uwezo mkubwa wa kunusa, hivyo
ukifukia kitu hata chini anaweza kukitambua
endapo tuu kina harufu ya damu damu.
 
Viumbe hawa wakijihakikishia akiba ya chakula
katika himaya zao, basi hufanya sherehe na
sherehe zao huwa na ufanano na sherehe za
binadamu, hucheza, hufurahi, hufanya ngono
na ugomvi huzuka pia wakati huo watoto wote
hufichwa ndani ya nyumba.
 
Fisi jike huweza kupiga dume mpaka likahama
nyumba, na hutumia sana ujanja huu endapo
jike linataka kuishi na mchepuko wake ndani.
 
WANYAMA WABABE KWA FISI

Fisi ni mnyama mnyonge sana na ni mnyama
ambaye karibia wanyama wote wawindaji ni
wababe kwake, kinachowasaidia ni hali ile ya
kutembea makundi makundi yaani kifamilia,
ndio huwafanya na wao waonekane kidogo
wanajiweza.
 
UKIKUTANA NAYE UFANYE

Kwanza kaa ukijua fisi sio mnyama wa
kumchezea, naye ana uwezo wa kukurarua vile
vile, usijeanza fikiria zile hadithi za shule ya
msingi ukamchukulia pia, sungura mwenyewe
akimuona anafungua njia vibaya sana,
japokuwa si kiumbe anayevamia moja kwa
moja, huuma kwa kuvizia, jihami vya kutosha
na uwe na silaha nzuri kama fimbo nzito, mawe
yenye ujazo mzito, na usimpe nafasi ya
kumuonesha unamuogopa japokuwa kicheko
chake chaweza kukutia hofu Mara dufu.
 
Ukumbuke anapotoa sauti hizo, wenzie
wanaposikia hujua kina jambo, hivyo hakikisha
haumpi nafasi hiyo..
 
Usisubutu kumvizia fisi kwa nyuma, namna
pekee ya kujirinda hurusha kinyesi chake kwa
ghafla na atakuacha ukiwa umechanganyikiwa
huku yeye akikimbia.
 
Uoga kwake huisha akiwa na njaa Kali, kwa
mfano hawezi kumuwinda binadamu mkubwa,
lakini litokeapo suala la njaa Kali huwa hajali
umri wa mtu.
 
Watoto wake wanapofikisha umri wa miakamiwili mama yao huwatimua, wakajitegemee.
 
Fisi dume halitakagi kusikia habari za watoto,
huwa linaamini ni Mali ya jike, hivyo hanaga
nao msaada kabisa.
 
Back
Top Bottom