Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Unapolitaka jambo kwa dhati, pigania. Usikate tamaa hata kama kila kitu kinaonekana kuwa hakina matumaini. Na pale utakapoanza kupoteza imani, jiulize: ‘Miaka 10 kutoka sasa, nitajuta kwamba sikujaribu mara moja tena?.
 
Tabia ya mtu huonekana si kwenye maneno, bali kwenye maamuzi anapokasirika, anapokuwa na pesa, au anapokuwa juu kuliko wengine.
 
Usiwahi kulipiza kisasi kwa mtu aliyekuumiza. Ukijua thamani yako, utanyamaza na kuendelea — kwa sababu karma inafanya kazi kimya kimya.
 
Maamuzi ya leo ni matokeo ya kesho, amua vyema upate mema: japo kukosea ni njia ya kujifunza pia.
 
Usijitoe kupita kiasi kwa watu wasioona thamani yako. Maji hayamiminwi kwenye kikombe kilichopasuka. Toa kwa busara, jitoe kwa wanaojali.
 
Dunia haitakupenda kwa kuwa mkweli. Mara nyingi, ukweli huumiza, na wengi hupenda uongo mzuri kuliko ukweli mchungu. Lakini kuwa mkweli bado ni ushindi wa ndani.
 
Kitu kinachoumiza zaidi siyo kutoeleweka, ni kueleweka vibaya na wale uliowapigania sana. Sio kila mtu atakuelewa, hata kama utamgusa kwa upendo.
 
Ni jambo la kusikitisha kwamba watu wengine hawajali kusikia upande wako wa ukweli, kwa sababu walichosikia kutoka kwa wengine tayari kinawapa sababu ya kukuona kwa mtazamo walioupenda
 
Akili nyingi huzungumza, lakini busara huchagua wakati sahihi wa kunyamaza.Mara nyingine ukimya wako ni sauti yenye heshima zaidi.
 
Busara ni pale unapotambua kwamba si kila jambo linahitaji majibu, na si kila mtu anahitaji kujua upande wako wa hadithi.Wengine wanafurahia kukuchafua bila sabuni.
 
Maisha hayatangazi masomo yake, yanafundisha kwa ghafla — kupitia watu, huzuni, na vikwazo.Ukiyavumilia, yatakuweka mahali palipo bora kuliko ulipotoka.
 
Kubadilika ni uchungu. Kukubali kuwa uliyekuwa jana siyo bora ni ugumu.Lakini ndipo maisha huanza kusogea mbele
 
Maisha sio mashindano, ni safari ya mtu na ratiba aliyopangiwa na Mungu. Usichome mafuta kushindana na waliobeba upepo.
 
Inawezekana kabisa huruma yako ndio chanzo cha matatizo unayo yapitia, Kuwa makini na unao Wahurumia.
 
Kumwamini mtu ni kama kumkabidhi Bunduki, Anaweza kukupiga risasi ama Kukulinda.
 
Back
Top Bottom