Unapolitaka jambo kwa dhati, pigania. Usikate tamaa hata kama kila kitu kinaonekana kuwa hakina matumaini. Na pale utakapoanza kupoteza imani, jiulize: ‘Miaka 10 kutoka sasa, nitajuta kwamba sikujaribu mara moja tena?.
Dunia haitakupenda kwa kuwa mkweli. Mara nyingi, ukweli huumiza, na wengi hupenda uongo mzuri kuliko ukweli mchungu. Lakini kuwa mkweli bado ni ushindi wa ndani.
Ni jambo la kusikitisha kwamba watu wengine hawajali kusikia upande wako wa ukweli, kwa sababu walichosikia kutoka kwa wengine tayari kinawapa sababu ya kukuona kwa mtazamo walioupenda
Busara ni pale unapotambua kwamba si kila jambo linahitaji majibu, na si kila mtu anahitaji kujua upande wako wa hadithi.Wengine wanafurahia kukuchafua bila sabuni.
Maisha hayatangazi masomo yake, yanafundisha kwa ghafla — kupitia watu, huzuni, na vikwazo.Ukiyavumilia, yatakuweka mahali palipo bora kuliko ulipotoka.