Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kila mtu ana uhuru wa kuwa kile anachotaka kuwa. Ni juu yako kujenga ujasiri na kufanya kazi kwa bidii, ili kufika pale unapotaka kuwa.” - Mike Adenuga
 
Utu uzima huja na mengi. Kuna shinikizo la kazi. Kuna kugeuza uzoefu kuwa kipato. Kuna ombwe la ndoto na uhalisia. Kuna muda na familia. Kuna migogoro mingi isiyosemwa. Kuna mipango kutetereka. Kuna kuishiwa. Kuna kujitafakari kunakohitaji kujitenga. Kuna kupumzika. Mtu wako wa karibu kutokupatikana haimaanishi hakujali.
 
Kadhalika, utu uzima hubadilisha mazungumzo. Kila unachokisema kinamkumbusha mtu historia fulani. Maumivu alo’wahi kupitia. Usaliti alo’wahi kukutana nao. Kuna imani zisizobadilika. Kuna tabia mtu anazopambana nazo bila mafanikio. Kuna hatia. Kuna aibu. Kuna fedheha. Ombwe. Unyonge. Ukiona mtu kakuweka pembeni haimaanishi hakupendi.
 
Kuna umri ukifika watu wanakuwa wanajua mengi yanayokuhusu lakini hawawezi kukuambia. Inaweza ikawa ni kukuheshimu, kukuogopa, kuamini unajua unachokifanya lakini saa nyingine ni ile tabia ya kusubiria waje waseme, ‘hili tulilijua mapema.’
 
Unazingua, kwa mfano, hawakuambii. Wanaambiana. Unawakera hawakuambii. Wanaambiana. Unaharibu hawakuambii. Wanaambiana. Unafanya vizuri wanaogopa kukuvimbisha kichwa. Hawakuambii. Wanaambiana. Ukiwa na uwezo wanasita kukusifia. Wanaambiana wenyewe kwa wenyewe.
 
Ukichunguza kile watu wanachoambiana, ukifuatilia ‘maneno maneno’ yanayokuhusu lakini usiyoambiwa moja kwa moja, utajua kwa nini mambo yanakuendelea hivyo yanavyokuendea. Kuna ukweli mwingi unaokuhusu na watu wanashindwa kukufikishia. Kuna hisia nyingi hazikufikii lakini zipo na watu wamezitunza wanasubiri ujichanganye kidogo waje waseme ‘tulijua.’
 
Usiwafanye watu wakawa na mengi wanayoyajua na hawawezi kukuambia ukiwepo. Kadhalika, ingawa tunapenda kuonekana wakamilifu, usikwepe sana kujua upande wako wa pili ambao ndio hasa wasifu wako unaotumiwa na watu kufanya maamuzi mengi yanayokuhusu. Unachokwepa kukijua huenda ndicho kinachoamua umbali utakaokwenda.
 
Mafanikio ni bahati. Kadri unavyojituma kwenye ubunifu, kutafuta maarifa, uthubutu na uvumilivu ndio bahati yako inaongezeka.” - Ruge Mutahaba
 
Back
Top Bottom