Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Si kila mtu anayatazama maisha kwa jicho lako. Usiwaswage watu kuamini unachokiamini.
Si kila mtu anahitaji kuwa na elimu uliyonayo.
Elimika kwa unyenyekevu.
Si kila mtu anahitaji kuelewa hicho unachokielewa. Jifunze kwa kutulia.
 
Si kila mtu anapenda madaraka ulo’nayo.
Cheo kisikuondolee ubinadamu.
Si kila mtu anahitaji kwenda ukikoenda wewe.
Pata ‘exposure’ (safisha macho) kwa utulivu.
Si kila mtu anahitaji mpenzi.
Shiba mapenzi bila maonesho.
 
Tunakuwa wasumbufu kwa wengine kwa kufikiri kila mtu anahitaji kile tunachohitaji sisi, anapigana vita tunayopigana sisi, anasumbuliwa na kile kinachotusumbua sisi. Tunasahau kuwa watu wana haki ya kuchukulia poa vile tunavyotumia nguvu kubwa kuvipata tukifikiri ni vya maana.
 
Kuna umri ukifika watu wanakuwa wanajua mengi yanayokuhusu lakini hawawezi kukuambia. Inaweza ikawa ni kukuheshimu, kukuogopa, kuamini unajua unachokifanya lakini saa nyingine ni ile tabia ya kusubiria waje waseme, ‘hili tulilijua mapema.’
 
Back
Top Bottom