Kadhalika, mtihani mwingine ni pale mwenzako anapokukosea. Je, unapozungumza naye unampa kweli nafasi ya kueleza kwa nini amekosea? Je, anapokiri makosa una uwezo wa kumsamehe na kumpa nafasi ya kuanza upya au hukomi kumkumbusha kosa kila mnapotofautiana? Je, ikifika mahali mkashindwa kuelewana, huenda habadiliki na umechoka, unaweza kusitisha uhusiano kwa kuheshimiana na kusitiriana?