Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Acha maneno
 
Liked
 
Word
 
Leo naona umekuja kivingine kabisa. Safi sana!
 
TUJENGE NIDHAMU

Kukosa nidhamu katika mambo madogo usitegemee kuwa na nidhamu katika mambo makubwa hata siku moja.

Kuna watu utawasikia nitakuwa na nidhamu nikiwa na cha kwangu, mwingine utasikia nitakuwa na nidhamu nikipata kitu flani. Wacha nikukumbushe kitu ndugu chochote ambacho unakifanya kinahitaji nidhamu kwenye vitu ambavyo ni vya kwako na vingine ambavyo sio vya kwako pia.

Usitegee uheshimu biashara yako na za wengine usiziheshimu alafu ufanikiwe.Haujawahi kujiuliza kwanini watu wanakuwa na biashara na hata hazisongi mbele? mtu unakuwa na bidhaa lakini unamaneno mabaya kwa mwenzako ambaye anafanya vizuri alafu unarudi kumwomba Mungu akusaidie ufanikiwe, utafanikiwa namna gani? au huyo Mungu ambaye unamwomba ni Mungu wa namna gani ambaye unamaliza kusali alafu unatoka kwenda kufanya maovu kwa mwenzako kwasababu anafanya vizuri? wewe ni mfanyabiashara wa namna gani ambaye unaenda kanisani au msikitini ukitoka tuu siku inayofuata ni kupiga majungu biashara ya mwenzako. Nidhamu ni kitu muhimu sana katika kila jambo ambalo unalifanya. Bila nidhamu hauwezi kuwa na kitu kikasimama kukuwakilisha wewe vizuri bila nidhamu utakuwa mtu wa kufanya mambo ilimradi ufanye au ilimradi uonekane umefanya.

Kuna watu wanadhani nidhamu ni kuheshimu tuu kitu wanachokifanya au biashara ambayo anaifanya, hapana hiyo sio nidhamu.

Ukiwa na nidhamu utafanya mambo yako kwa usahihi na huo usahihi wake ni kuhakikisha unaheshimu na biashara za watu wengine ambao hata ndo wameanza, ukiwa na nidhamu utaheshimu taratibu za kazi za watu wengine bila kujali umewapita au wamekupita namna gani.

Bila nidhamu unaweza kufika juu unapotaka lakini kukaa hapo juu na watu kukuelewa inaweza kuwa kazi ingine ambayo inaweza kukufanya kushuka tena chini kuitengeneza nidhamu yako.Nasema hivi kwasababu kunawengine wanaweza kutumia uongo wakawa kwelii na hela vizuri, kunawengine wanaweza kutumia uongo kupendwa na watu kweli, kunawengine wanaweza kutumia uongo kudanganya wateja wao kwelii ili wenzake wasiwapate lakini tambua uongo unaweza kukupeleka unapopataka lakini usipate vile ambavyo ulidhani utavipata hiyo sehemu uliyofika mfano unaweza kukosa heshima kwa watu, kutokukumbukwa kwa uzuri wa mambo ambayo uliyokuwa ukifanya mana hakuna zuri ulilolifanya kwa nidhamu n.k


Usijenge nidhamu kwa kuweka matabaka au usijenge nidhamu ya kuigiza. Unaweza kuwa na maono au malengo makubwa mbeleni lakini kama huna nidhamu kwa mambo madogo ni ngumu sana kuweza kuyafikia mana sifa ingine ya nidhamu ni kufuata utaratibu ambao umejiwekea na kuufanyia kazi bila kushusha au kuharibia wengine mazingira yao.

Ni muda wa mimi na wewe Kujenga Ndoto zetu kwa kuwa na nidhamu ambayo ni mwonekano wa maono yetu ya baadae.




Sent from my Apple iPhone 5s using JamiiForums Auto-reply Mobile app
 
Thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…