Muwe makini pia guys, matapeli ni wengi sana, Kuna mkaka aliwahi andika bandiko kwa mtandao fulani kua anatafuta mke, wadada wakatuma maombi kama yote, kumbe yule kaka mi mume wa mtu na tena hana hata kazi,
Aliwatafuna wadada uwiiii, yaani walikua wanasafiri tena kwa nauli zao kumfata bonge la bwana, wengine walikwea hadi pipa , nyie wanawake tuko desperate na ndoa, kaka aliwala hadi huruma, na wengine akawa anawaambia niko na ratiba ngumu, nitumie nauli nipande ndege nikufate, wajinga walituma, aseeee
Guys msicheze na hisia za wadada, kama hauko na uhitaji waachie wenzio wenye nia, wadada usimtumie mtu pesa eti atakuja kunioa, watu wanalizwa sana, wengine wanaoa hadi ndoa feki aseee...
Mtu ana mke na watoto yuko bize amekomaza shingo mtandaoni anatafuta mke, matapeli ni wengi, trust no one, usitume picha zako ovyo, take time kumjua mtu, usiende meetings kiholela mtaishia kuliwa na ndoa mtaiskia kwa bomba, tena mtaliwa bureeee,
Be carefully and all the best....