Uzi maalum wa kutafuta mchumba. Weka Wasifu wako hapa upate wa kuanza naye maisha (njoo tuishi/tuyajenge)

Uzi maalum wa kutafuta mchumba. Weka Wasifu wako hapa upate wa kuanza naye maisha (njoo tuishi/tuyajenge)

Habari wanajamvi hususani wanawake mlio singo na mnahitaji mwenza/mme wa maisha. Nami nimehamasika kuja uwanja huu kwani nimepata shuhuda kadhaa za waliofanikiwa kupata wenza humu jamvini.

Kiufupi nina kiu kubwa sana ya kupata mke kwa ajili ya kuanzisha na kuendeleza familia. Nishajipanga kimaisha na kisaikolojia.

Nina akili timamu na ninafahamu kuwa mwenza wa maisha anapatikana popote pale, tena nawashukuru waliotuletea platfom hii kutusaidia sisi ambao hatupati fursa hizi sehemu nyingine kwa sababu mbalimbali.

WASIFU WANGU
Jinsia; Me
Umri; Miaka 34
Kazi; Nimejiajiri pia nimeajiriwa
Elimu; Masters in Finance and Investment
Dini; Mkristo LC
Makazi; Dar Es Salaam

Mengineyo
Nina mwili wa wastani mrefu kiasi kimo futi 5 inchi 10, uzito kg 72. Sura ya kawaida na nina bald head( uwalaza)

Ni husband material kwa kwel, napenda sana familia, kujituma na kuwekeza ili kujiletea maendeleo


WASIFU WA NINAEMHITAJI

1. Umri awe miaka 25-30
2. Elimu angalau diploma
3. Kazi; Awe ameajiriwa/Kujiajiri. Ila hata kama hana kazi kwa sasa, nitamtafutia shughuli ya kufanya maana naamini katika kazi.
4. Dini; Napenda awe mkristo hususani dhehebu la LC, RC, au pentecoste
5.Makazi; Dsm, au awe tayari kuja kuishi Dsm
6.kabila; napendelea zaidi wa nyanda za juu kusini maana mmi ndio napotokea.
7. Awe na umbo la wastani, kama ni mnene asiwe mnene kupita kiasi

Mengineyo
Napenda mwanamke anaejitambua na anaejua wajibu wake kama mama wa familia

Napenda mwenye kiu ya maendeleo, asiwe mtu wa tamaa.

Napenda pia awe mshauri na mwenye kuona mbali kupitia ya leo(mwenye maono)


Nawakaribisha wenye nia. Karibuni


MAWASILIANO; PM YANGU IPO WAZI HADI NITAKAPOFANIKIWA

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe unafaa kabisaa kuwa mume!
 
Me.....
Name : classified
Edu level : Advance Diploma
Age. : 26
Status. : single and serious.
Religion : Muslim(not radical muslim)
Region. :Same Milimani (Mamba myamba)
Consumings: Not alcoholic, i smoke Weed and love to eat...
Hobbies. : Partying , swimming, movies Etc
Financial: Employed but Dying to start my own shit(lets start 2getha, start small is my philosophy,hata iwe biashara ya [emoji534] poa tu)


Her....
Name : i dont care
Edu lvl : At least Certificate
Age. : Below 26 yrs
Status: single and serious...
Religion: Muslim Fear of God...
Region. :Any But Mtz only.
Hobbies: any
Consuming : Any but specific weed
Financially : Employed or self employed is gud but if not we will start 2getha...


Watsup # 0694 263 118
njoo tuyajenge.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umri - 29-34
Elimu -Degree ya mtaani
Dini - Mkristo
Rangi - Mweusi tii
Umbo - Miraba minne
Kazi - Kujiajiri na kuajiriwa

NINAYEMUHITAJI

umri - 22-27
Elimu - ajue kusoma na kuandika
Dini - mkristo atapendeza zaidi
Rangi - nyeusi tii narudia tena nyeusi tii
Umbo - awe mfupi kipotabo
Kazi - asiye na ajira

Kigezo cha muhimu kuliko vyote awe ametokea ukanda wa pwani..mwenye sifa hii atapata kipaumbele cha kuweka ndani mapema..pia aliyeshindikana mtaani yaani wale wanawake wajeuri, watukutu kila aina ya balaa wameshapitia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: amu
Hahahaa.. haiwezekani kiongozi... Huwa napenda kuishi maisha ya uhalisia na si kuigiza
Sasa mkuu ulikuwa wapi siku zote??? Humu kuna uzi mmoja niliandika wa kutaka kumuunganisha bachelor mwenzangu mmoja binti mwenye sifa za kuwa mke wa mtu maana mm sikuwa na uwezo wa kumuoa na kwa nilivyokufuatilia ukimjibu huyo mdau anayekufundisha mbinu haramu za uzinzi nikajikuta nimekupa points za kuwa bachelor mwenye focus na ulichokiandika..

Dah sema basi tena ndo haikiwa rizq yako kuna mdau nilishamuunganisha na ameshafuata taratibu zote soon anaenda kutoa mahari na ana mzuka kuwa hataki funga ndoa ya Corona(kimyakimya)anataka watu wale mpunga so atasikilizia Corona ipoe kisha afunge ndoa..

AnywaY tuendelee na mapambano bachelor mwenzangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom