NILITUNGA HILI SHAIRI BAADA YA KUFANYAGA MAPENZI NA MWANAMKE MWENYE HIV . MWANZO NILIAMINI SIJAPATA BILA KUPIMA ILA BAADAE NILIANZA KUUMWA VIGONJWA VISIVYOELEWEKA YANI MWILI ULINICHEZEA AKILI NILIKONDA NILICHOKA SANA
NIKAAMINI TAYARI MPAKA NIKAENDA NIKITAKA NIPEWE DAWA TU NI SEPE WAKAGOMA KUNIPA MPAKA WAPIME NILIKUBALI WANIPIME NIKIWAAMBIA WANAPOTEZA MUDA BURE . NILIPIMWA ZAIDI YA MARA TATU HAPO NI ZAIDI YA MIEZI SITA TOKEA MARA YA MWISHO KUKUTANA NAE HUWEZI KUAMINI SIKUWA MWATHIRIKA WA HIV . KUNA AHADI NYINGI NILIMPA MUNGU KABLA YA KUELEKEA KUPIMA NAAMINI NDIO MUUJIZA ULIOTOKEA
BURIANI
Buriani waungwana, limenipata dubwana,
Mapema tunaagana, Ningali bado kijana,
Maumivu yanibana, kuandika nangangana,
Buriani waungwana, limenipata dubwana,
Sina wa kumpa lawama, hata Zerea kimwana,
Akijua sana vyema, kalizoa Dubwana,
Kama na kosa kusema, nisamehe tu Rabana
Buriani waungwana , limenipata dubwana,
Simanzi imenitanda, Giza ti likitanda,
Siwezi tena kutenda, siku nzima tu kulala
Nimechoka nimekonda, nipumzike ndio sala
Buriani waungwana , limenipata Dubwana
Malengo yamezimika, kama nta yayeyuka,
Sijui kama ntafika, hata kesho kunyanyuka,
Tumaini lakatika , kiama kinanifika,
Buriani waungwana, limenipata dubwana
Kama vile mnaniona, mwovu kupita kipimo
Ajuae ni Rabana, kwake nafanya ungamo
Nazidi kuchoka sana, niondoke tu nilimo
Buriani waungwana, limenipata dubwana
Kwaherini Marafiki, wangu wa nema na dhiki,
Hata wale wanafiki, chekeni sasa mna haki
Dubwana hakabiliki, kifo hakiepukiki,
Buriani waungwana, limenipata dubwana
Wazazi na ndugu zangu, musiwe na mfadhaiko
Ni mapenzi yake Mungu, hakunalo badiliko,
Pokeeni tu japo chungu, kwake nipate pumziko
Buriani waungwana, limenipata Dubwana,
Kwaherini Duniani, Tuonane bandarini,
Kwaherini jamiini, na hata kule Twitani,
Na kote mitandaoni, niwaage kwa amani
Buriani waungwana, Tutaonana baadae
Buriani waungwana, limenipata dubwana, Mapema tunaagana, Ningali bado kijana, Maumivu yanibana, kuandika nangangana, Buriani waungwana, limenipata dubwana, Sina wa kumpa lawama, hata Zerea kimwana, Akijua sana vyema, kalizoa Dubwana, Kama na kosa kusema, nisamehe tu Rabana Buriani waungwana ...
www.jamiiforums.com