Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Hatukwenda pamoja, yule mwanamke nilimpenda sana ila yeye hakuwa na upendo wowote kwangu, alijua khali yake, ila alifanya makudi, ameambukiza wengi na isingekuwa Mimi angeambukiza wengi zaidi, ila baada ya kumgundua nikamwambia ukweli kuwa TUMEPOTEZA but we can live happily tuoane, AKAKATAA, hivyo nilitangaza sana kwa watu wa pale kambini na vijana wengi walisalimika kwa kile nilichokifanya, japo yupo mmoja ndo alikuwa form six likizo, huyu aliambukizwa waziwazi. Iliniuma sana maana alikuwa kijana mdogo, natamani kungekuwa na sheria ya kuzuia hili, maana yule mwanamke alikuwa mtu mzma, ni aibu na huzuni sana kumfanyia vile yule dogo. Anyway baada ya watu kumsakama alijitundika. Hatunaye tena.​
Aisee nimekuelewa mkuu ila kuhusu sheria ipo wazi kwamba kumuambukiza mtu ukimwi kwa makusudi ni kosa kisheria huyo dogo wa form six angeweza kufungua kesi ingewezekana kabisa
Ila ndio ilishapita na huyo Dada katangulia mbele ya haki.
Yote kwa yote nakupongeza sana kwa huo moyo wako kwa kweli Mungu akubariki
 
Kaka Mimi sio advertiser, lakin jaribu kumcheki Docta Tr Msigwa akutibu kwa 100% then kacheki VIRAL LOAD then ishi, ARV zitakuletea madhara apo baadae mkuu
 
Na waume wengi tukiotulia tunaletewa na Wake wanaorukaruka nje
Kweli kabisa ukitulia mwenza wako anaeruka analeta ila sio sana sababu wanaume hawachubuki sana ubaya mpaka maji maji ya wanaume mbegu zinaweza kukupa virusi kama hajaanza kutumia ARV
 
Imebidi niende kum Google huyo demu.
Tafuta Colombiana muvi utamuona akiwa mdogo
FB_IMG_1711169009109.jpg
 
Aisee nimekuelewa mkuu ila kuhusu sheria ipo wazi kwamba kumuambukiza mtu ukimwi kwa makusudi ni kosa kisheria huyo dogo wa form six angeweza kufungua kesi ingewezekana kabisa​
Ila ndio ilishapita na huyo Dada katangulia mbele ya haki.
Yote kwa yote nakupongeza sana kwa huo moyo wako kwa kweli Mungu akubariki
The issue is watu wahawezi kujitolea kushtaki, that's why hakuna case kama hiyo. But ni haki, na anastahili kuadhibiwa mtu amuambukizaye mwenzie makusudi.​
 
Akhsante kwa ushauri mdogo Angu🙏😎
Kaka Mimi sio advertiser, lakin jaribu kumcheki Docta Tr Msigwa akutibu kwa 100% then kacheki VIRAL LOAD then ishi, ARV zitakuletea madhara apo baadae mkuu
 
Mimi ukimwi ni nimepima sina ila sitosahau
Jinsi nilivyoshudia ukimwi ukitekeleza mauji ya mtu nilimpenda sana MAMA ANGU MZAZI TENA DAKTARI ALIKUWA

Mama angu alikuwa yupo hapo wilaya inaitwa mafinga huwa kuna ukimwi sana tulihamia mwaka 1996 kutoka dar es salaam kwa miaka mingi nilishuhudia vifo vya majirani walivyokuwa na ukimwi sababu mama alikuwa daktar wengi walikuwa wakija nyumbani kutibiwa na kupewa ushauri miaka ile ya 90s hadi 2000s mwanzoni

2010 na kumi nikahama jumla mafinga na kuja dar kutafuta maisha baada ya kumaliz masomo yangu ya degree .....2013 tukamzika babangu mzazi ambae alichana na mama mama angu mwaka 96 sasa baada kutoka msibani nikamuuliza mama huyu baba kafa kwa HIV vipi ww utakuwa mzima akanijibu mimi ni mzima mwanangu

2016 nilikuwa na safari kwenda china kwa ajlii ya business zangu nikarudi mafinga kwenda kumuaga sasa alinituma kitu nikachukue chumbani kwake naingia nakuta ARV kitandani moyo wangu ulisononeka sana nakumbuka nililia sana ila mama angu akasema usilie ni jambo la kawaida nakumbuka akiniangalia kwa macho ya aibu huku pia akijikaza sababu alinipenda sana koz mimi wa mwisho kwetu

2020 kipindi ch korona mama angu mzazi anapapalaizi baada ya kupigwa stroke for two years anakuwa kitandani

2022 mama angu anaingia deadliest stage ya Ukimwi AIDS..Hapa sasa ndo nilijua ukimwi mbaya alitokwa na vidonda mgongo mzima sababu alikuwa kapalalaize hivyo bed sores zilimuandama sana.....wewe anakonda ....mno kumbuka mimi hapo miaka hiiyo mitatu natumia hela zngu binafsi nilitumia zaidi millioni 30 hadi niliyumba kidogo kiuchumi sababu ya kuuguza mgonjwa safari za magari dawa kwenda rufaa mara week nyumbani mwezi hospital ...mara hali hadi mipira mara awe kichaa mara awe mzima nyie ukimwi balaa stage ya mwisho ile

2022 machi hali inakuwa mbaya mgonjwa ni amepalalaize mwili umebaki kichwa tu....vidonda kila kona ndugu zake wananyanyapa yaani ilibidi nimkodi nesi wa kike anisaidie kazi kusafisha vidonda kila siku 20000tsh....... then mach 2022 mama akafariki .....taarifa ya kufAriki kwakwe ilinikutia bar nikiwa na marafika zangu nilikaa kimya

Nilirudi nyumbani nikasema pole na mama angu nilikupenda sana bora umekufa kuliko ulivyokuwa unateseka maana mgongo ulikuwa kama nyama buchani hakuna ngozi......

Nikasema nitakukumbuka daima na kukupenda daima then nikalala zangu nikatafuta dereva wa kuniendesha hadi mafinga iringa nikampa laki mbili nikajaza mafuta tukaondoka .....njiani nae dereva nusu aniue pale kitonga anasisinzia nikamwambia unajua mimi naenda msibani afu unaleta usengeee ...nikachukua chuma mwenyewe nikaendesha hadi mafinga

2022 machi 25 tukamzika mama angu mzazi msibani nilikuwa nauchungu kuwa sito muona tena ila kifo sometimes ni muhimu kwa mateso aliyoyapata kifo ilikuwa bora kuliko kuishi .....maana miguu mgongo ilikuwa ni nyama za buchani tu

Hadi leo hii hakuna siku inapita simkumbi mama angu mzazi

So wagonjwa wa ukimwi mezeni dawa pia hakikisheni vizuri

Pia serikali iweke sheria kwa hospital au madaktar kuwaua kwa maksudi kwa agizo la mgonjwa mwenyewe endapo stage aliye fikia hawezi pona maana inakuwa ni mateso sio kuumwa ....hasa kwa wagonjwa wa kansa mara nyingi madaktar hujua kuwa flan haponi wanabaki wanazuga tu na mgonjwa anateseka bure na maumivu makali yasio na mwisho.....
Dada naomba nisaidie kazi tu nitakushukuru sana
 
Ilikuwa mwaka 2001 nilikuwa na mchumba wangu akawa anahitaji kunivalisha Pete mwenyewe alikuwa hajatulia na Mimi nilikuwa na kamsimamo Fulani hivyo akaona asinisumbue aendelee kula nje

Sasa bwana mazingira ya kazi yakanifanya nikajikuta nimeliwa na kijana mmoja wa hapo kazini ambaye muda mwingi tulikuwa tuko wote ofisini ndio alienitoa bikira. Huwa sipendi kabisa ule Uzi wa kula tunda kimasihara nililiwa kizembe sana.

Mchumba akataka tuweke mipango tuvalishane Pete nikasema iliyopo nikapime kwanza nikijikuta salama basi nimlazimishe naye akapime acha 😭😭😭kwanza. Nilienda kupima nikaambiwa niende baada ya wiki kipindi hicho nafikiri hata angaza ilikuwa haipo.

Baada ya wiki nikaenda 😭😭😭😭 yule mama sijui yupo baada ya yale maswali Yao akaniambia umeadhirika yasikia yasikufike nililia sana nikiangalia Sina CV ya wanaume kichwani nikaanza kuomba sala za mwisho mwisho😂😂😂

Yule mama akañiambia kama una Imani unaweza kupona Kuna watu nimewapima nikakuta wagonjwa ila baada ya kuombewa walipona.

Akaniagizia Kwa mchungaji mmoja yule mchungaji alinisaidia sana japo hata Leo nikimwona siwezi mkumbuka.

Mchungaji alianza kuniambia Jinsi yeye alivyokuwa ameadhirika mwili umeishia alikonda Kila akienda kupima anakuta Bado anao wakati mwingine analazwa hivyo akawa ni mtu wa maombi sana muda mwingi hata ibada ikishatoka yeye anabaki pale madhabahuni akimlilia Mungu. Siku moja akaenda akapima akakuta mzima kabisa akapima baada ya miezi mitatu tena akakuta mzima.

Basi akaniambia usimwambie mtu watu watakutia hofu, omba tu Mungu peke yako. Nilikuwa naomba nyie nilikuwa nalia na Mungu nikakataga mawasiliano na Mchumba nikawa Mimi na Mungu tu nikapima mara ya kwanza nikapata negative nikapimaga tena niko negative.

Ila jamani asikuambie mtu dalili zote unaziona kisa tu umeujua ukweli baada ya vipimo kuonekana Sina nikawa sawa kabisa.

Nikajaga kuolewa na mtu mwingine kabisa japo Mchumba hakuamini na aliyenikula sijuagi yuko wapi niko na familia yangu. Kupona kupo ila ujitoe hasa hasa
Nakubali kabisa, hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu. Amen
 
Wadudu wanaupita uzi kwa mwendo wa ngiri mkia juu.

Eneweiz kama hujazaliwa nao pole kwa mahangaiko ya dunia hii mkuu.

Kwa vijana kama huwezi kuacha ngono na unataka kupiga mbususu safely, tembelea vituo vya watoa huduma hospitali zote za serikali upatiwe dawa kinga(PREP) ni bure, hii itakusaidia kucheza mechi salama hata ukipiga nyama kwa nyama na muathirika.

Dj piga OCG ~ Ni kazeze.
Tunza afya kwa maendeleo ya Taifa.
 
Back
Top Bottom