Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

💯💯
Wadudu wanaupita uzi kwa mwendo wa ngiri mkia juu.

Eneweiz kama hujazaliwa nao pole kwa mahangaiko ya dunia hii mkuu.

Kwa vijana kama huwezi kuacha ngono na unataka kupiga mbususu safely, tembelea vituo vya watoa huduma hospitali zote za serikali upatiwe dawa kinga(PREP) ni bure, hii itakusaidia kucheza mechi salama hata ukipiga nyama kwa nyama na muathirika.

Dj piga OCG ~ Ni kazeze.
Tunza afya kwa maendeleo ya Taifa.
💯💯
 
X wangu ameenda kutafuta maisha mgodini namuonea huruma
 
Kuna jamaa tunakunywa nae pombe kila siku,wanaomjua wanasema ana ngoma,jamaa kajidhira kabisa,nadhani hata dawa hanywi yule.
 
Usiniambie habari za kupanic weee😂 kupanic lazima
Ukipanic umeisha, we hata ukiupata chukua hela nenda Serena hotel tuliza mawazo hata wiki, then come and face the reality.😂 anyway wacha nipeleke gari yangu kwa fundi maana haiponi duh sijui kuna ukimwi wa magari?
 
Ukipanic umeisha, we hata ukiupata chukua hela nenda Serena hotel tuliza mawazo hata wiki, then come and face the reality.😂 anyway wacha nipeleke gari yangu kwa fundi maana haiponi duh sijui kuna ukimwi wa magari?
Kwahiyo ulifungua uzi kutusema tusiokua na magari kumbe wewe mwenyewe una kagari kamoja.
 
Mimi ukimwi ni nimepima sina ila sitosahau
Jinsi nilivyoshudia ukimwi ukitekeleza mauji ya mtu nilimpenda sana MAMA ANGU MZAZI TENA DAKTARI ALIKUWA

Mama angu alikuwa yupo hapo wilaya inaitwa mafinga huwa kuna ukimwi sana tulihamia mwaka 1996 kutoka dar es salaam kwa miaka mingi nilishuhudia vifo vya majirani walivyokuwa na ukimwi sababu mama alikuwa daktar wengi walikuwa wakija nyumbani kutibiwa na kupewa ushauri miaka ile ya 90s hadi 2000s mwanzoni

2010 na kumi nikahama jumla mafinga na kuja dar kutafuta maisha baada ya kumaliz masomo yangu ya degree .....2013 tukamzika babangu mzazi ambae alichana na mama mama angu mwaka 96 sasa baada kutoka msibani nikamuuliza mama huyu baba kafa kwa HIV vipi ww utakuwa mzima akanijibu mimi ni mzima mwanangu

2016 nilikuwa na safari kwenda china kwa ajlii ya business zangu nikarudi mafinga kwenda kumuaga sasa alinituma kitu nikachukue chumbani kwake naingia nakuta ARV kitandani moyo wangu ulisononeka sana nakumbuka nililia sana ila mama angu akasema usilie ni jambo la kawaida nakumbuka akiniangalia kwa macho ya aibu huku pia akijikaza sababu alinipenda sana koz mimi wa mwisho kwetu

2020 kipindi ch korona mama angu mzazi anapapalaizi baada ya kupigwa stroke for two years anakuwa kitandani

2022 mama angu anaingia deadliest stage ya Ukimwi AIDS..Hapa sasa ndo nilijua ukimwi mbaya alitokwa na vidonda mgongo mzima sababu alikuwa kapalalaize hivyo bed sores zilimuandama sana.....wewe anakonda ....mno kumbuka mimi hapo miaka hiiyo mitatu natumia hela zngu binafsi nilitumia zaidi millioni 30 hadi niliyumba kidogo kiuchumi sababu ya kuuguza mgonjwa safari za magari dawa kwenda rufaa mara week nyumbani mwezi hospital ...mara hali hadi mipira mara awe kichaa mara awe mzima nyie ukimwi balaa stage ya mwisho ile

2022 machi hali inakuwa mbaya mgonjwa ni amepalalaize mwili umebaki kichwa tu....vidonda kila kona ndugu zake wananyanyapa yaani ilibidi nimkodi nesi wa kike anisaidie kazi kusafisha vidonda kila siku 20000tsh....... then mach 2022 mama akafariki .....taarifa ya kufAriki kwakwe ilinikutia bar nikiwa na marafika zangu nilikaa kimya

Nilirudi nyumbani nikasema pole na mama angu nilikupenda sana bora umekufa kuliko ulivyokuwa unateseka maana mgongo ulikuwa kama nyama buchani hakuna ngozi......

Nikasema nitakukumbuka daima na kukupenda daima then nikalala zangu nikatafuta dereva wa kuniendesha hadi mafinga iringa nikampa laki mbili nikajaza mafuta tukaondoka .....njiani nae dereva nusu aniue pale kitonga anasisinzia nikamwambia unajua mimi naenda msibani afu unaleta usengeee ...nikachukua chuma mwenyewe nikaendesha hadi mafinga

2022 machi 25 tukamzika mama angu mzazi msibani nilikuwa nauchungu kuwa sito muona tena ila kifo sometimes ni muhimu kwa mateso aliyoyapata kifo ilikuwa bora kuliko kuishi .....maana miguu mgongo ilikuwa ni nyama za buchani tu

Hadi leo hii hakuna siku inapita simkumbi mama angu mzazi

So wagonjwa wa ukimwi mezeni dawa pia hakikisheni vizuri

Pia serikali iweke sheria kwa hospital au madaktar kuwaua kwa maksudi kwa agizo la mgonjwa mwenyewe endapo stage aliye fikia hawezi pona maana inakuwa ni mateso sio kuumwa ....hasa kwa wagonjwa wa kansa mara nyingi madaktar hujua kuwa flan haponi wanabaki wanazuga tu na mgonjwa anateseka bure na maumivu makali yasio na mwisho.....
Kaka umeongea kishujaa sana tena mno sana ukimwi ni hatar achana na hawa wanaosem ukimwi ni kama malaria hawajashuhudia ila kwa tulio wahi kuona wagonjwa hawa ni hatar mno kuna mama mmja alikuwa bonge la mtu mwili nyumba
Kumbe amepata ngoma alafu akawa anagawa kwa vijana wadogo yaani ukiona tako hutoki sio powa siku hazigandi chuma ikaanza kumla imemla mtu wa kilo 110 kwenda juu akabaki kilo25 nilishangaa sana mpk kutembea mtaani anaona aibu anajificha yaani kapukutika kabaki mifupa mifupa anakohoa kama mbuzi nywele zimenyonyoka kama kinda la ndege nyie acheni kabisa
 
Binafsi huu ugonjwa kamwe siwez upata...Narudia tena siwez upata..lakin kwa mlio nao sio ugonjwa wa kutisha kero kwenye kumeza dawa...usipate sukari...cancer au figo zifeli alafu dailisis ije...NB wagonjwa wote hapo nimeshawauguza kwa gharama zangu bila kuchangiwa au serikali kutia mchango wake....ikitokea nimecomment uzi wa mwana jamii forum yeyote tuheshimiane...na sio mwajiriwa mimi hata bima zenyewe kwenye hayo magonjwa zinadunda...nipo blw 33 years...na katika hao nilio wauguza mwenye ukimwi ndio yupo owk mpaka sasa tna na TB ilimpiga akawa wa kesho au masaa afariki..but ukimuona now...aisee kuwen makini
Kwa nini unasema huwez kupata coz kuna njia nying za kupata ukimwi sio lazima kufanya mapenzi tu ndio utapata
 
Back
Top Bottom