Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Kwa wale ambao wanauliza ni mambo gani au dalili gani zinakufanya upime?

Jibu ni moja tu Ukiwa na wasi wasi na nyendo zako basi pima,ukihisi una mashaka basi pima

Kiufupi kupima ukimwi unastahili medali ya dhahabu,,huwezi kuepuka hofu nadhan kwasababu ugonjwa wenyewe unatia hofu
 
😭😭😭
Pole sana mkuu.
 
Binafsi huu ugonjwa kamwe siwez upata...Narudia tena siwez upata..lakin kwa mlio nao sio ugonjwa wa kutisha kero kwenye kumeza dawa...usipate sukari...cancer au figo zifeli alafu dailisis ije...NB wagonjwa wote hapo nimeshawauguza kwa gharama zangu bila kuchangiwa au serikali kutia mchango wake....ikitokea nimecomment uzi wa mwana jamii forum yeyote tuheshimiane...na sio mwajiriwa mimi hata bima zenyewe kwenye hayo magonjwa zinadunda...nipo blw 33 years...na katika hao nilio wauguza mwenye ukimwi ndio yupo owk mpaka sasa tna na TB ilimpiga akawa wa kesho au masaa afariki..but ukimuona now...aisee kuwen makini
 
Mkuu,
Kuna mtu kwa takriban robo Karne sijawai mwona anameza dawa Ila anadunda
Some people were very strong
Namaanisha watumiaji wamwisho yaani wagonjwa wanazipata bila kudaiwa fedha, la sivyo wasio na kipato wangepata shida.
Hili linafanyika duniani kote.

Wajibu mojawapo wa serikali ni kumrudishia mwananchi faida ya kodi yake.
 
K
Ni msemo, kwenye maisha, ukiona watu wako wa karibu mliokuwa pamoja tangu enzi za ujana na utafutaji na struggle za kutoboa kwenye maisha wanadondoka kwa mfululizo Jua muda sio rafiki

Noted unknown
Kuna watu walikuwa wanamsema vibaya jamaa na mkewe baada ya kugundulika wana virus vya ukimwi.
Cha ajabu wale woote waliokuwa wanamsema wameshatangulia mbele za haki halafu jamaa na mkewe bado wanadunda na wana watoto wenye afya tele.
Maisha.....................
 
Kuna manzi nilimuaproach, akanipa sharti zito sana la kupima VVU kwanza, dah, lakini kwakuw nlikuwa namkubali sana nkasema fresh.

Alisema twende wote, nkapiga moyo konde nkasema poa, siku ya tukio kachimba hajatokea, nkasema haina shida.

Nkampigia sababu kibao, akasema kesho twenda, nkasem sawa.

Kesho tena kachimba, dah, nkasema ni noma. Ikabidi npime pekeangu.

Nashukuru nkajikuta fresh, dah, skuamini maana nshapuyanga sana.
Yule manzi ikabidi nimpotezee maana anatoa masharti ambayo ye mwenyewe hayawezi, ni snitch
 
Dah kwa madaktari humu, nilikutana na mwanamke siku 40 zilizopita, lakini nilipima siku ya 26, 31, na 40 nikawa niko fresh, kuna haja ya kusubiri miezi mitatu? Maana nasikia hivi vipimo vya sasa huko senstive sana week mbili tu kitu kinasoma.
Japo nimeulizia na nimeangalia kwenye website mbalimbali kwamba hawajawahi kuexperience mtu yupo negative kwa siku 40 then uje kubadilika baada ya miezi 3.
 
Safi..huu ndio uwanaume sasa...
 
Pole sana mkuu, pia akhsante kwa ushauri.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Ushaur wangu kuwa navyo kwako mbona si gharama..mimi sio docta bt home kwangu nina vipimo vingi sana kwa usalama wa familia yangu
 
Mshukuru mungu kwa hilo, Linda afya yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…