Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Uzi maalumu kwa watu wenye UKIMWI

Mkuu, Dawa ni chungu au angalau kidogo zina uperemende ndani yake? Maana kunywa dawa asubuhi, mchana na jioni hii ratiba sijui inawezekanaje.
Swali lako limenichekesha eti chungu. Nimewahi meza hizo dawa mara 2 as PEP jibu ni kua unameza mara moja kwa siku ila hazina uchungu labda uzimung'unye changamoto niliyoona ni vidonge vikubwa kwa ambao hatupendi kumeza dawa ni changamoto sana.

Pia kwa sasa regime mpya inayotumika ni TLD ambayo haina shida na unaweza meza muda wowote mtakaokubaliana na muhudumu wa afya wakati wa kuanza matibabu.
 
Daah aisee hongera kwa kujitambua.
Mimi mara ya mwisho nilipima 2021, nilikua -ve.

Ila migodini naskia ni habari nyingine kabisa.
halafu migodini haijawahi kutajwa kuwa kuna maambukizi makubwa, walitaja madreva malori malori tu huko barabarani. Siku hizi kampeni za kupima kwa hiari zimepungua huenda maambukizi yapo juu sehemu nyingi licha kuwepo kwa dawa za kufubaza
 
Wakati nipo songea 2008 kuna binti nilimpata tukawa wapenzi alikuwa na miaka 16 na nilikuwa na nia nimuoe kwasababu mtoto alikuwa mzuri na muelewa mno,,,basi ikawa tunasex sana tena bila kondom kwasababu niliwaza mtoto kama yule sio wakumtilia shaka,,,na ikapita miaka miwili tupo kwenye mahusiano ila kila mmoja anaishi kwake na yeye alikuwa anaishi na shangazi yake,,sasa kuna siku nilienda mtaani kwao kuna kitu nilimpelekea sasa tukawa tumesimama jirani na shule fulani hivi tunapiga story,,,kumbe kuna mtu mmoja akatuona pale na siku ya pili akanijia dukani akaniambia ndugu yangu yule binti unajuana nae kiundani? Nikamjibu hapana nipo kwenye mchakato wa kumtongoza jamaa akaniambia yule binti ana ukimwi kazaliwa nao, aisee nilivurugwa mno na nililia sana nikanyanyua simu nikampigia yule binti nikamuuliza kumbe wewe una ukimwi? Aisee dogo akaniambia tu ukweli huku analia kuwa ni kweli ni muathirika ila alikuwa anaogopa kuniambia nisije kumuacha na wakati mimi ndie nilikuwa namuhudumia kila kitu na binti maisha yao yalikuwa magumu mno,,,Sasa washkaji wakaniona kabisa nimevurugwa akili nipo kama mwehu kwasababu nilimpigia mama yangu simu nikamwambia mimi mwanao nina ukimwi kwahiyo sipo mbali nitakufa.ila baada ya miezi miwili nikaenda kupima nikakutwa nipo fresh aisee nilifurahi mno kama chizi na nikampigia yule binti simu nikamwambia nipo fresh binti alifurahi mno,, kwakufupisha story ni kwamba yule binti kafariki 2015 kwa ajali ya gari
 
Hapana mkuu! Nina tatizo la kusumbuliwa na vitu vibaya au vya kusikitisha
Huwa siangalii movie za huzuni, sisikilizi story za kusikitisha nikifanya hivyo tu naweza kukaa hata wiki moyo na akili vinasikitika nakosa utulivu
Dah pole sana mkuu , jaribu kukabiliana na hiyo shida yako , kwa sababu kwnye hii dunia kuna mengi ya huzuni mno utakabiliana nayo , jifunze namna ya kukabiliana na hofu yako .
 
P

Punguza ngono zembe, sijui kwanini wanawake wengi hamsistz matumizi ya condom, mnamuachia mwanaume ndo aamue. 🤐
Aisee nilijua ni Mimi tu naokutana nao labda,kumbe ni wengi.
Ukimuuliza vipi tutatumia condom anasema sijui wewe mwenyewe
Na hapo mmekutana hata mwezi haujaisha
 
Binafsi huu ugonjwa kamwe siwez upata...Narudia tena siwez upata..lakin kwa mlio nao sio ugonjwa wa kutisha kero kwenye kumeza dawa...usipate sukari...cancer au figo zifeli alafu dailisis ije...NB wagonjwa wote hapo nimeshawauguza kwa gharama zangu bila kuchangiwa au serikali kutia mchango wake....ikitokea nimecomment uzi wa mwana jamii forum yeyote tuheshimiane...na sio mwajiriwa mimi hata bima zenyewe kwenye hayo magonjwa zinadunda...nipo blw 33 years...na katika hao nilio wauguza mwenye ukimwi ndio yupo owk mpaka sasa tna na TB ilimpiga akawa wa kesho au masaa afariki..but ukimuona now...aisee kuwen makini

Kaka temea mate chini usisime huwez pata kuna watu wameupata mpaka unashangaa kumbe wengi tunapata kwa haohao tunao wapenda na tunao waamini haswaaa !!!!
 
Back
Top Bottom