Kuna kaka mmoja tukipataga muda wa kuongea ananitania haya maswali
1. Luckyline hivi unavyo jitunza hivi wewe ni mwanamke wa aina gani?
2. Luckyline ni kwamba unaogopa wanaume au ni nini hasa?
3. Luckyline mbona mzuri tu au unabagua sana wanaume?
4. Sasa unavyojitunza hivi ikitokea ukapata mwanaume akakuambukiza ukimwi utafanya nini?
Jibu ni moja ninalompa, mimi nashukuru sikuzaliwa na ukimwi kama wengine wanavyoupata kwa kuzaliwa nao, sio kwamba naogopa wanaume mimi nina sababu.
Mungu mimi nimejinyima starehe zote za duniani, sijawahi fanya umalaya wa aina yeyote hapa duniani.
Kaka niliyempenda alipo niacha niliumia nililia nikajifungia ndani wiki mbili, nae sikuwahi fanya mapenzi nae bila kinga nae nishahidi hata akisoma hapa.
Maumivu yale niliyaugua miaka 2 na miezi 9, nikajaribu kwingine nae hatukufika mbali nilimuona sio muoaji, nae sikushiriki nae bila kinga.
Nikapata mwingine nakili ingawa nilimpenda kuliko wote ila sikuwahi kukutana nae live, siku napanga nimtembelee, nikagundua anaishi na mwanamke ndani ndo maana hakutaka nisafiri kwenda kwake.
In short sijawahi ingia mahusiano na mtu ambae naona hafai kuwa mme.
Wale wachache niliyo ingia nao mahusiano sijawahi kushiriki tendo bila kinga.
Kwa umri nilio nae nilitakiwa niwe na msululu wa wanaumwe nashukuru Mungu hata watano hawazidi na kati yao wengine hatukufika hiyo hatua.
Sio kwa mimi ni malaika au mwema hapana ninataka mwanaume wa kuishi nae, staki mwanaume wa kuniletea ukimwi na kuondoka.
Maisha yangu nimejinyima nimejihudummia mwenyewe, kipindi sina kazi niliangaika na biashara, hela niliyoipata nilijilipia kodi, wakati mwingine na mtaji unapungua dah, nilipitia kipindi kigumu, natongozwa naogopa kutoka out na mtu nikiogopa nikila pesa zake nalipa nini.
Kwangu ndani sina kitu chochote ambacho ni pesa ya mwanaume hakipo.
kalamu haiozi Mungu ni mwema kanipa kijikazi najihudumia sio kwamba staki kuhudumiwa, naogopa nikihudumiwa namlipa nini?
Maisha yangu yote niliishi nikiamini mm nitakuwa mke wa mtu na kamwe hili litatimia who know? May be soon!!
Wanaumwe wa siku hizi si waoaji akiona kama sisi ambao tunajitafutia basi anataka aje azalishe aondoke, staki hilo linitokee.
Point ni kwamba tamaa zimewaponza wadada kupata ukimwi, waume za watu wanatumia dozi linakupa hela linakuambukiza unaishi kwa stress.
Nina mifano mizuri marafiki zangu wengine ni wagonjwa nawaonea huruma.
Nimejitunza sana ukimwi siwezi kuunywa kwenye maji, huyo mwanaume nitakae ishi nae akiniambukiza ukimwi, hicho kisasi nitakachompa kitaumiza ukoo wake wote.
Maisha yangu yote nimejinyima starehe za mahusiano, kutendwa kumenifanya nichukie wanaume wa kiafrica.
Mungu naomba uendelee kunilinda usije nipa mwanaume akaniltea ukimwi, maana mimi siwezi kuutafuta hiyo haiwezekani mpaka hapa nilipofikia.
Mdada au mkaka utakae soma hapa, acha tamaa ukimwi ni mbaya, ingawabkuna magonjwa makali kuliko hata ukimwi, fanyan kazi pata hela zako usitegemee hela ya mtu, hela ya mtu ni majuto itakupeleka kaburini.
Umwa magonjwa mengine ila sio ukimwi wa kijitafutia.
Nyie wakaka usimuamini mwanamke kufanya nae mapenzi bila kinga, utakatisha ndoto zako, wanawake wenzangu wana tamaa, wanamiliki wanaume 4 kwa mkupuo, hamko salama kaka zangu.
Mungu wape faraja wote walio pata ukimwi kwa kuwaamini wenza wao.
Kaka dada linda sana afya yako vile vidonge vya kumeza sila siku vinatesa vinaweza kukuletea any side effect mbaya, mifano ninayo mingi sana.
N.b sitafuti mwanaume humu coz am done with african men, huu uzi umenigusa, maisha yangu niligopa mahusiano moja wapo ikiwa ni kuogopa kupata ukimwi na kunifanya single mom.
Hata hao wachache nilio ingia nao mahusiano wengine hatukufika mbali maana hawakutaka kinga nikajiondoa nashukuru wengine walikuwa ni waelewa.
Mungu ni mwaminifu nina historia ya kipekee ya mahusiano. Hizi starehe ni za hapa duniani bora niwe salama.
Dada kaka ishi ndoto zako ukimuomba Mungu.