Uzi maalumu kwa wenye ndoa

Uzi maalumu kwa wenye ndoa

Siri ni kuwa marafiki,mpate muda wa kukaa kupiga story kama marafiki mpaka mnajikuta mnaongelea tofauti zenu kwa namna ya utulivu bila kuhamaki na hapo mnadumisha upendo katika ndoa yenu!

Makwazo yatakuwepo lakini mkiyashinda ndoa ni njema sana!

Hakuna raha kama uone jioni baba anarudi na watoto wanafurahia uwepo wake na weekend yupo nyumbani anacheza na kuonyesha upendo kwa watoto,raha sana jamani asikwambie mtu!

Hakuna kitu kizuri kama bond between baba na wanae mana kwetu wanawake bond huwa ipo automatic toka wakiwa tumboni!

Mungu awatunze na kuwapa maisha marefu wanaume wote wanaojali wake zao na watoto wao,hawa ni hazina kwa taifa!

Much respect to you all😍
 
Huu uzi yule Establishment asiuone.. yule tokea kaoa ndoa yake inatimka vumbi. Hakumpata wa ubavu wake,, asije hapa na mambo yake negatively akawatisha vijana
 
Kama upo kwenye ndoa na unafurahia, basi huu uzi unakuhusu ili tuweze kubadilishana uzoefu wa namna gani ya kuishi na wenza wetu kwa furaha. Kupitia maoni mazuri yatakayotolewa hapa inawezekana tukawavuta wa wale ambao hawataki kuoa/kuolewa.
Karibuni sana
Huu uzi auone UMUGHAKA
 
Ila kubwa nililojifunza kwenye ndoa ni msiwe na vinyongo. Ni sumu kubwa sana. Inatengeneza chuki ya chinichini siku viki erupt unasema hee huyu kamuuaje mwenzake hivi?

Kubwa ni kwamba mwenzako akikukosea ongea in a calm way sasa ndo ukute mume ana mfumo dume ukifungua tu mdomo anaona umemtukana mayuuuuu🤣🤣🤣 mlioolewa na wakoloni poleni.
 
Hakika, hata dunia iumbwe tena, wakisema tukatafute wengine sijui wawe na nini. The bar is set too high. Wanaume wapendeni wake zenu jamani kuna guilt huwa inatupata when a man is too caring hutamani hata kuuliza makosa if you find one. Ndoa ni furaha ndoa ina afya
tuliambiwa tuoe/kuolewa ili tupate utulivu wa nafsi, mimi ever since nimeolewa nikawa namwambia mume hivi tulichelewa wapi, ndoa yenye amani ujue na Mungu yupo, watu wanachukulia tu vitu juujuu, ukiiheshim ndoa ukaitumikia utayaona matunda yake,
 
tuliambiwa tuoe/kuolewa ili tupate utulivu wa nafsi, mimi ever since nimeolewa nikawa namwambia mume hivi tulichelewa wapi,ndoa yenye amani ujue na Mungu yupo, watu wanachukulia tu vitu juujuu, ukiiheshim ndoa ukaitumikia utayaona matunda yake,
Natamani amani hii iishi milele. Kama hakuna sababu ya ugomvi basi bora kukaa kimya. Hongera kwa kuwa na ndoa njema. Mungu azidi kuwafungulia heri
 
Ila kubwa nililojifunza kwenye ndoa ni msiwe na vinyongo. Ni sumu kubwa sana. Inatengeneza chuki ya chinichini siku viki erupt unasema hee huyu kamuuaje mwenzake hivi...
Mimi hio ndio natumia sikai na jambo rohoni na wala hakai na jambo rohoni naweza nisimwambie ana kwa ana lakini nikamtumia kitabu kwenye msg na mtu anajua kweli nimeharibu sio kwa gazeti hili na maisha yanaendelea.

Kuna ile wanakumbushia yaliopita mkigombana kidogo tu mtu anakumbushia ya mwaka jan wajue lililopita limepita halina nafas tena na itamfanya mwenzie aone kumbe ana kinyongo bado hata mkisameheana anajua unafake kumsamehe
 
By the way,,, uzi kama huu tayari upo humu jukwaani!!
 
Natamani amani hii iishi milele. Kama hakuna sababu ya ugomvi basi bora kukaa kimya. Hongera kwa kuwa na ndoa njema. Mungu azidi kuwafungulia heri
aamyn, atufungulie heri sote halaf mkishakua wazazi yale mapenzi mnayahamishia kwa watoto jinsi wanaona mnavyoongea bila kukwaruzana mnataniana watoto unawaweka sawa akili zao kuliko nyumba yenye malumbano watoto hukosa amani,
 
Na kingine nilichosahau, namshukuru Baba naniii kwa kunipa familia yenye upendo hivi. Mama mkwe wangu jamani Mungu akuweke. Kuna koo zina amani jamani. Watu wana upendo sio wa kawaida ni wana umoja. Kwani nilimpa nini Mungu. I do not deserve hiki kipande cha huku. There is peace all over.

Wanawake, smart intelligent and loving men exist. Msikae mnasoma hizi nyuzi za matusi juu ya wanawake humu mkadhani all men are trash. Mda mwengine hata wao ni toxic kwa wake zao. Pray to God upate wa type yako
 
Ni vema kwa nyakati hizi tukakubaliana kama tulivo kubaliana kwenye kuabudu dini zetu iz mbili pendwa,kwa maana kwamba kama kunawatu wanashikilia msimamo wakuto kuoa waendelee na msimamo wao ,vile vile wanao amini kwenye kuoa nao waendelee na huo msimamo wao. Nimefikia kusema haya baada ya kusoma nyuzi nyingi jamvin humu na hakuna siku suruhu ilipatikana.

Na hata ukijikita kuzitafakar hoja za pande zote mbili utaona zinamashiko japo wanao sisitiza kuoa huwa na ziada ya dini na jamii kuwa kama huta owa unaweza kuonekana muhuni na mabaya yote utapakaziwa kulingana na mitazamo Yao. Lakin kwa dunia ya digital hii vijana na hoja Yao ya kataa ndoa na kampeni zingine zinazofanana na hili pia huwa na hoja chache za msingi, mfano swala la usaliti kwa pande zote mbili ,uchumi,upatikanaji wa ngono kirahis ni tofauti sana na nyakati zile.

Kwa sasa ngono inapatikana sehemu zote nyakati zote na kwa mtu yeyote..yani mpaka anaye hitaj shoga anapata 🤣🤣. Ko kiukwel mahusiano kwa nyakati hizi kwa vijana hayana maisha marefu . Pia tusisahau matatizo ya nguvu za kiume ni shida kwa vijana siku hizi.

Nimalize kwa kusema ni mwaka sasa naishi na mwanamke aliye nizalia mtoto ko siwez sema ndoa nirahis au lah!! Naomba nijipe muda bado mapema kwangu kukoment mazur au mabaya ya ndoa .
 
Back
Top Bottom