Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

View attachment 3121418

Ndugu watanzania kupitia Uzi huu nitakuwa Kila siku Alfajiri ninatuma mstari maalumu wa maombi Kwa wale waombaji wa asubuhi. Ufunguapo Uzi huu kuanzia saa nane kamili usiku utakutana na maneno yatakayokuongoza na kuchochea nguvu ya maombi.

MSTARI WA KUSIMAMIA
Zaburi 90:14 " Utushibishe Asubuhi kwa fadhila zako. Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote"
LUGHA;

Tunaomba Uzi huu uchangiwe Kwa Lugha nzuri yenye staha ili kuwasaidia wapenzi wa maombi ya Asubuhi kupata sehemu ya kutumiana jumbe na kuombeana. Haitakuwa busara kama hauamini katika maombi ukatukana au kukashifu jambo linaloweza kusababisha Uzi kufungwa.

Mbarikiwe na karibuni kwenye Uzi huu maalumu kwaajili ya maombi ya Asubuhi.

Asubuhi ya Leo 10/10/2024 post #13 au bofya hapo chini kupata mstari wa leo
Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Leo 11/10/2024 post #49
Bofya kiungo hapo chini kwaajili ya maombi ya leo.
Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

New. 11/10/2024
Kwa watakao penda kupokea ujumbe wa maombi mstari wa KUSIMAMIA Kwa njia ya Text za kawaida ama watsup. Ni vyema tutawasiliana PM Kwa mujibu wa sera ya faragha ya Jf. Pia kuanzia Jumatatu ijayo yaani 14/10/2024 tutakuwa na watsup group mahsusi Kwa maombi. Kwa wenye uhitaji tuwasiliane PM.
Mbarikiwe
14/10/2024
Nawaombeni radhi Kwa ukimya wa siku mbili tatu hizi maombi mazuri siku zote hayakosi changamoto tuzidi kuombeana aidha Kwa Wana watsup tuzidi kujisajili... Tukutane muda wa maombi ya moto ! Usibaki nyuma!
15/10/2024 post#114 Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

16/10/2024 post no 23 Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Leo 18/10/2024
Page #140 Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Leo 19/10/2024
Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Post #144
Leo 21/10/2024
Leo 23/10/2024
Amen
 
Attachments

  • 1729827698138.jpg
    1729827698138.jpg
    382 KB · Views: 2
Baba katika jina la Yesu tunasema asante kwa ulinzi wako umetulinda mpaka kufikia siku hii ya leo si kwa uwezo wetu bali kwa nguvu zako tunaomba ulinzi wako ukaendelee kuwa upande wetu watesi wetu wakashindwe katika jina la Yesu AMINA
 
View attachment 3126078Amkeni katika maombi. Mstari wa kusimamia 2 nyakati 7:14 " ikiwa watu wangu, walioitwa Kwa jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kutafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya,n basi nitasikia Toka mbinguni na kuwasamehe dhambi Yao na kuiponya nchi Yao."
Asubuhi hii tunaalikwa na Baba kwenda mbele zake Kwa unyenyekevu na kuomba, Bwana atasikia kutoka mbinguni. Tafakari mstari huu Kwa utulivu Kisha tuingie katika maombi.
Amen
 
Zaburi inayotupa uhakikisho wa ulinzi wa Mungu ni Ile zaburi ya 91

Zaburi 91​

1Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
2Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
3Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
4 Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
5 Hutaogopa hatari za usiku,
Wala mshale urukao mchana,
6Wala mapigo yajayo usiku,
Wala maafa yatokeayo adhuhuri

Soma na kushika Neno lote
 
prayer for ma family protection
 
Attachments

  • 1729830140632.jpg
    1729830140632.jpg
    289.9 KB · Views: 2
Amen
 
Attachments

  • 1729830180328.jpg
    1729830180328.jpg
    552.9 KB · Views: 3
Bwana Yesu asifiwe wapendwa

Kuna jambo nataka niwashirikishe wapendwa Mungu anapenda kuomba kwetu kuwe na reference kutoka katika biblia utabarikiwa unapomuomba Bwana Yesu akusaidie jambo lolote kwa kuwa na reference
mfano unaugonjwa na unataka kupona kwenye kuomba kwako usisahau kumkumbusha Bwana kutoka katika Neno hili kutoka

Zaburi 107:20
Hulituma neno lake, huwaponya,
Huwatoa katika maangamizo yao.

Muambie Bwana wewe ulisema utalituma neno lako kutuponya Leo hii nipo mbele zako nami ninaamini kwa Neno lako nitapokea uponyaji maana wewe Bwana ni muaminifu kama ulivyosema katika

2 Wathesalonike 3:3
Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu.

Jaribu kuomba mahitaji yako yote mbele za Bwana ukiwa na reference utaona matokeo makubwa sana Roho Mtakatifu atakupeleka kwenye viwango vingine vya maombi utajua chanzo Cha tatizo lako na tatizo litaisha gafla tu kimiujiza lakini pia Roho Mtakatifu ataanza kukupa muongozo mzuri kwa kila hitaji unalotaka

Bwana Yesu awabariki sana
 
Naomba Bwana atupe kibali siku ya kesho tukutane tena hapa tutakuwa na jambo hili

Kitu cha kwanza sala na maombi yote yaliyofanywa na manabii nyakati tofauti tofauti za kuhitaji ushindi ,kuomba rehema, uponyaji maombi yote yawepo katika jukwaa hili

Kitu cha pili wiki hili nataka tufanye maombi tutembee na Neno katika kufanya maombi
Kila mtu baadae atatakiwa kupost mstari au mistari ya biblia aliyoishika kichwani ili basi wiki hili lote tutembee na Neno katika kufanya maombi yetu mbele za Bwana Yesu
 
Wewe ni mwanga na uzima, neema na rehema, haki na haki, na kujazwa na upendo na nguvu. Hebu mioyo yetu ikukaribie leo. Tunakutafuta kwa mioyo yetu yote kwa sababu tunajua kwamba tamaa zetu zinapatikana na kutimizwa ndani yako. Tunataka kukujua wewe, Bwana.

Neno linaloniongoza katika maombi yangu siku ya Leo ni kutoka katika kitabu cha yeremia na mithali

BWANA anaonekana zaidi pale tunapomtafuta kwa bidii sana

Yeremia 29:12-
Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza.

Yeremia 29:13
Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu

Mithali 8:17
Nawapenda wale wanipendao,
Na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
 
Inuka na uangaze kupitia maombi muda huu. Tuombe juu ya familia na ndoa zetu.

Baba katika Jina la Yesu, tunazileta ndoa zetu mbele zako. Wewe ndio uliyemuumba Adam, ukamuumba na Hawa, halafu ukawakutanisha, ukawaunganisha. Hakuna kufika kwa Hawa bila kufika kwako kwanza. Hakuna kufika kwa Adamu bila kufika kwako kwanza (Mwa 2:22). Basi Bwana Mungu, kwa kutambua hili tupe kujua muunganiko wetu ni imara ikiwa tu wewe ndo uko katikati yetu, juu yetu, pembeni yetu, mbele yetu, nyuma yetu. Wewe ni yote katika yote.

Tunaombea kubebana katika madhaifu yetu. Tupe kuelewa mapendeleo ya wenza wetu na ondoa mbegu za ubinafsi ndani yetu. Wewe PEKEE ndie unaeweza kumbadilisha mwanadamu, tunaiomba amani ipitayo fahamu zote ipate kuhifadhi mioyo yetu ili kubeba interests za wenza wetu ili tusiamshe magomvi ndani ya familia kisa kutopendelea mwenza mmoja anachofanya. Tunaomba mtazamo mpya juu ya interest za wenza wetu ambao utatuongoza namna ya kufikiri, kuomba na kuyabeba mambo wanayopendelea ili tu TUSIUMIZWE na petty things zitakazoharibu mahusiano yetu na wewe Mungu wetu.

Lakini pia tunaomba juu ya past relationship ambazo tulishakuwa nazo na zinaleta trauma katika ndoa zetu za sasa. Tunavunja kila muunganiko wa kale from any past relationship iwe ulikuwa mzuri au mbaya, spiritual tie yoyote, emotional tie yoyote, ivunjike hiyo nira katika Jina la Yesu. Kwakuwa tumeamua kuwa pamoja kwa mapenzi yako wewe ulietukutanisha basi hayo ya kale YAMEPITA sasa tumekuwa wapya katika Kristo. Tunaandikwa na wino usiofutikwa wa Roho Mtakatifu na tunasonga mbele katika kuyaendea mapenzi yako katika ndoa zetu.

Tunafuta neno kutengana, talaka, nimechoka nataka kuondoka, I give up, from mioyo yetu na ndoa zetu. Kama tuliapa kwamba kifo tu kitutenganishe basi NENO HILO TU LIKASIMAME katika maisha yetu ya ndoa. Tusaidie tuwe mfano bora kwa watoto wetu ili baadae waje kuwa watu bora katika jamii na taifa kwa ujumla. Tunaomba hekima ya namna ya kufanya maamuzi ili tusikosee kamwe.

Tunayo mengi ya kuomba baba lakini kwa ujumla tunakabidhi ndoa zetu kwako be our LORD AND MASTER. Lastly, tuokoe na KILA neno baya na kutuhifadhi hata tufike kwenye ufalme wako wa mbinguni (2Tim 4:18). Ni katika Jina la Yesu, tunaomba na kupokea kwamba yamekuwa yetu...AMEN.
 
Asante, Bwana, kwa baraka ulizonipa juu ya maisha yangu . Umenipa zaidi kuliko nilivyofikiria. Umenizunguka na watu ambao wananiangalia kila wakati. Umenipa familia na marafiki wanaonibariki kila siku kwa maneno na matendo mema.
Zaburi 138
Zaburi 86
 
Yeremia 31:26
[26]Basi, nikaamka, nikaangalia; na usingizi wangu ulikuwa mtamu kwangu.

Tuombe:
Baba mtakatifu uketiye mahali pa juu palipoinuka, tunakushukuru kwa ulinzi wako usiku wa leo, maana tulilala kama tuliokufa hakujua lolote lakini kwa neema yako umetuamsha tena siku ya leo tarehe 28/10/2024, tunaomba uwepo wako uende nasi, kama ulivyowapigania wana waizrael jangwani tunaomba nasi Bwana usituache, tunawasogeza wenzetu ambao ni wagonjwa mbele zako ukawape neema ya uponyaji kwa damu ya Yesu, wajane na yatima na wote wenye shida mbali mbali Mungu ukahusike maana umesema unashugulika na mambo yetu.

Tunaomba kwa ajili ya siku ya leo, tunaikomboa kwa damu yako, tukikataa roho za ajali na kila roho chafu kutoka kuzimu, ukabariki kazi za mikono yatu, utufungulie milango ya kupata riziki, ninaomba kwa jina la mwanao Yesu Kristo na kuamini, Amen
 
Back
Top Bottom