Inuka na uangaze kupitia maombi muda huu. Tuombe juu ya familia na ndoa zetu.
Baba katika Jina la Yesu, tunazileta ndoa zetu mbele zako. Wewe ndio uliyemuumba Adam, ukamuumba na Hawa, halafu ukawakutanisha, ukawaunganisha. Hakuna kufika kwa Hawa bila kufika kwako kwanza. Hakuna kufika kwa Adamu bila kufika kwako kwanza (Mwa 2:22). Basi Bwana Mungu, kwa kutambua hili tupe kujua muunganiko wetu ni imara ikiwa tu wewe ndo uko katikati yetu, juu yetu, pembeni yetu, mbele yetu, nyuma yetu. Wewe ni yote katika yote.
Tunaombea kubebana katika madhaifu yetu. Tupe kuelewa mapendeleo ya wenza wetu na ondoa mbegu za ubinafsi ndani yetu. Wewe PEKEE ndie unaeweza kumbadilisha mwanadamu, tunaiomba amani ipitayo fahamu zote ipate kuhifadhi mioyo yetu ili kubeba interests za wenza wetu ili tusiamshe magomvi ndani ya familia kisa kutopendelea mwenza mmoja anachofanya. Tunaomba mtazamo mpya juu ya interest za wenza wetu ambao utatuongoza namna ya kufikiri, kuomba na kuyabeba mambo wanayopendelea ili tu TUSIUMIZWE na petty things zitakazoharibu mahusiano yetu na wewe Mungu wetu.
Lakini pia tunaomba juu ya past relationship ambazo tulishakuwa nazo na zinaleta trauma katika ndoa zetu za sasa. Tunavunja kila muunganiko wa kale from any past relationship iwe ulikuwa mzuri au mbaya, spiritual tie yoyote, emotional tie yoyote, ivunjike hiyo nira katika Jina la Yesu. Kwakuwa tumeamua kuwa pamoja kwa mapenzi yako wewe ulietukutanisha basi hayo ya kale YAMEPITA sasa tumekuwa wapya katika Kristo. Tunaandikwa na wino usiofutikwa wa Roho Mtakatifu na tunasonga mbele katika kuyaendea mapenzi yako katika ndoa zetu.
Tunafuta neno kutengana, talaka, nimechoka nataka kuondoka, I give up, from mioyo yetu na ndoa zetu. Kama tuliapa kwamba kifo tu kitutenganishe basi NENO HILO TU LIKASIMAME katika maisha yetu ya ndoa. Tusaidie tuwe mfano bora kwa watoto wetu ili baadae waje kuwa watu bora katika jamii na taifa kwa ujumla. Tunaomba hekima ya namna ya kufanya maamuzi ili tusikosee kamwe.
Tunayo mengi ya kuomba baba lakini kwa ujumla tunakabidhi ndoa zetu kwako be our LORD AND MASTER. Lastly, tuokoe na KILA neno baya na kutuhifadhi hata tufike kwenye ufalme wako wa mbinguni (2Tim 4:18). Ni katika Jina la Yesu, tunaomba na kupokea kwamba yamekuwa yetu...AMEN.