Asante Mungu muumba wa mbingu na nchi kwa siku mpya tena, tunashukulu kwa kutupatia nafasi nyingine ya kurekebisha njia zetu, tunaomba nguvu zako zikatulinde tukaimalize siku salama, kwa upendo wako ukatujalie mahitaji yetu, tunasema asante kwa kutupigania vita vyetu, tumeuona mkono wako na matendo yako bwana ni makuu mno, kwa uchache wa maneno yetu tunaomba wingi wa neema zako,.
amen
.
Amkeni katika maombi. Mstari wa kusimamia "jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu,ila Mungu ni mwaminifu ambaye hata waacha mjaribiwe kupita muwezavyo, lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea ili muweze kustahimili"
1 wakorintho 10:13.
Tukumbuke Bwana mwenyewe ametuagiza tuombe "usitutie majaribuni Bali utuokoe na yule muovu"
Nawakaribisha tuombe juu ya majaribu. Ubarikiwe
Habari za kwenu wapendwa
Mwanzo nilikuwa nafikiri tuwe na ratiba ya kufanya maombi nimetafakari sana naona jambo hili litatubana sana kama sasa tunaelekea kipindi Cha uchaguzi inatubidi Tuombee sana amani na utulivu uendelee kudumu
Sasa tukishakuwa na ratiba itatulazimu tufuate ratiba na sio mambo mengine
Nazani kwa sasa siku hizi mbili m Tuombee sana taifa letu amani,utulivu na mamlaka zote kwa ajili ya kipindi hichi ambacho tunaelekea kipindi uchaguzi Tuombee ulinzi wa taifa lote Mungu anapendezwa na maombi haya na huwa yanajibiwa kwa haraka
2 Nyakati 7:14
Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
1 Timotheo 2:1-2
1. Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote
2. Kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na ustahivu.
Bwana, tafadhali uwe kati yetu tunapokusanyika kama chombo chako kuinua nchi yetu na viongozi wetu. Tafadhali linda nchi yetu dhidi ya mgawanyiko unaotia changamoto uwezo wetu wa kuishi maisha yanayokupendeza. Tetea walio hatarini na wasio na sauti, na ulete haki kwa wale ambao wamedhulumiwa.
Mithali 14:34
Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
Alfajiri ya Leo 10/10/2024
Amkeni katika maombi. MSTARI wa kusimamia.
Mathayo 7:9-11"Kuna mtu yupi kwenu ambaye mwanawe akimuomba mkate atampa jiwe? Au akiomba samaki atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, Je si zaidi sana baba Yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamuombao."
Ndugu Alfajiri ya Leo tunaalikwa kumpeleka Mungu mahitaji yake sawa sawa na Neno lake nae anaahidi kujibu Kwa wema sawa sawa na tutakavyo muomba. Tuamke tuendelee na maombi,
Barikiwa sana mtumishi wa Mungu.View attachment 3120433View attachment 3120436
Kila ukiwa unasikia Allah ahkbaru asubuhi au muda wowote jua ni kauli inayomtukuza Mungu kuwa Mungu Mkubwa na iwe sauti ya kwanza kuisikia kila uanzapo siku mpya aameen
Bwana, tafadhali uwe kati yetu tunapokusanyika kama chombo chako kuinua nchi yetu na viongozi wetu. Tafadhali linda nchi yetu dhidi ya mgawanyiko unaotia changamoto uwezo wetu wa kuishi maisha yanayokupendeza. Tetea walio hatarini na wasio na sauti, na ulete haki kwa wale ambao wamedhulumiwa.
Mithali 14:34
Haki huinua taifa;
Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote.
Ndugu watanzania kupitia Uzi huu nitakuwa Kila siku Alfajiri ninatuma mstari maalumu wa maombi Kwa wale waombaji wa asubuhi. Ufunguapo Uzi huu kuanzia saa nane kamili usiku utakutana na maneno yatakayokuongoza na kuchochea nguvu ya maombi.
MSTARI WA KUSIMAMIA
Zaburi 90:14 " Utushibishe Asubuhi kwa fadhila zako. Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote"
LUGHA;
Tunaomba Uzi huu uchangiwe Kwa Lugha nzuri yenye staha ili kuwasaidia wapenzi wa maombi ya Asubuhi kupata sehemu ya kutumiana jumbe na kuombeana. Haitakuwa busara kama hauamini katika maombi ukatukana au kukashifu jambo linaloweza kusababisha Uzi kufungwa.
Mbarikiwe na karibuni kwenye Uzi huu maalumu kwaajili ya maombi ya Asubuhi.
Asubuhi ya Leo 10/10/2024 post #13 au bofya hapo chini kupata mstari wa leo
Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Leo 11/10/2024 post #49
Bofya kiungo hapo chini kwaajili ya maombi ya leo.
Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
New. 11/10/2024
Kwa watakao penda kupokea ujumbe wa maombi mstari wa KUSIMAMIA Kwa njia ya Text za kawaida ama watsup. Ni vyema tutawasiliana PM Kwa mujibu wa sera ya faragha ya Jf. Pia kuanzia Jumatatu ijayo yaani 14/10/2024 tutakuwa na watsup group mahsusi Kwa maombi. Kwa wenye uhitaji tuwasiliane PM.
Mbarikiwe
14/10/2024
Nawaombeni radhi Kwa ukimya wa siku mbili tatu hizi maombi mazuri siku zote hayakosi changamoto tuzidi kuombeana aidha Kwa Wana watsup tuzidi kujisajili... Tukutane muda wa maombi ya moto ! Usibaki nyuma!
15/10/2024 post#114 Post in thread 'Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri' Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri
Zaburi 90:14 Utushibishe asubuhi kwa fadhili zako. Nasi tutashangilia na kufurahi siku zetu zote. Psalm 90:14 Oh, satisfy us early (in the morning) with Your mercy (steadfast love), That we may rejoice and be glad all our days! Amina nyingi mtumishi mjoli wa bwana
Amkeni katika maombi Leo, Maombi yenye majibu juu ya mahitaji yako,
Waebrania 4:16"Basi na tukaribie kiti Cha neema Kwa ujasiri ili tupewe rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji"
Ndugu Asubuhi ya Leo tunaalikwa kwenye kiti Cha enzi Kwa Ujasiri basi twende Kwa imani tukiamini yupo baba ambaye anasikia maombi yetu. Tuendelee na maombi mwana wa Mungu.
Maombi ya kuombea taifa ni maombi yenye nguvu sana haya ni maombi yenye kufungua mlango wako wa mafanikio na utajiri
Ukiamka usiku usisahau kuombea sana mambo haya kila siku
Ombea amani na utulivu
Ombea viongozi Mungu awape afya njema na hekima ya kuongoza
Ombea watu wote wenye mamlaka wafanye kazi kwa kutoa haki
Ombea rasilimali zilizopo katika taifa hili zinufaishe watanzania wote kwa usawa
Ndani ya kipindi kifupi tu utaanza kuona neema za Bwana Kuna mabadiliko utaanza kuyapata katika kazi au ajira uliyonayo
Haya hiyo ni nini? Ni uenda wazimu kubishania imani ya mapokeo, dini ziko nyingi sio uislamu na ukristo au Uyahudi tuu bali kuna zingine kama Budha na huwasikii wakileta mabishano.
Kila mtu aamini atakacho tusilazimishane maana mwishowe ni kuchakazwa kama kule Gaza bure!
Haya hiyo ni nini? Ni uenda wazimu kubishania imani ya mapokeo, dini ziko nyingi sio uislamu na ukristo au Uyahudi tuu bali kuna zingine kama Budha na huwasikii wakileta mabishano.
Kila mtu aamini atakacho tusilazimishane maana mwishowe ni kuchakazwa kama kule Gaza bure!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.