Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Amen
 
AMEN 🙏 🙏 🙏
 
AMEN
 
Naomba Bwana Yesu atupe kibali siku nyingine ya kesho asubuhi alfajili ili tukutane hapa jukwaani kwa ajili ya kuendelea kujifunza neno

Siku hizi mbili Tuombe Mungu ili Mungu aweze kutufungulia milango zaidi wiki hili katika
Mipango na malengo yetu
Kazi zetu
Biashara zetu
Ajira zetu

Tuendelee kufanya maombi lakini tuendelee na huu utaratibu wetu mzuri kutembea neno la Mungu biblia
 
Kuna mbinu hii ya uombaji ambayo itakusaidia sana kwako wewe unayeomba ili Mungu akupe mafanikio katika kazi/ajira unayoifanya

Kuna mambo mawili ambayo unatakiwa uombe sana unavyoamka asubuhi hii ukiwa faragha

1.Ombea kusudi Mungu aliloliweka ndani yako umeletwa duniani kufanya Nini? ombea lile kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako ili ukalifanye kwa ukubwa sana

Tunajifunza kutoka kitabu cha Yeremia hapa utaona kumbe kabla hata haujazaliwa Mungu ameshajua anakuleta kuwa nani huku Duniani

Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

2.Ombea sana kutumika katika kazi ya Mungu
Hiyo kazi/ajira uliyonayo Bwana amekuchagua wewe ili ajidhihirishe ukuu wake kwa watu wengine kwamba yeye ndiye mwokozi Bwana anataka hiyo kazi unavyofanya ikomboe maisha ya watu wengine watu watoke kwenye shida na umasikini hiyo kazi yako ombea sana kutumika ili watu wengine wapate mafanikio kupitia wewe Mungu atazidi kukuchagua wewe
Isaya 43:10
[10]Ninyi ni mashahidi wangu, asema BWANA, na mtumishi niliyemchagua; mpate kujua, na kuniamini, na kufahamu ya kuwa mimi ndiye; kabla yangu hakuumbwa Mungu awaye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine.

Kama ni mfanyabiashara ombea sana wateja wako wainuke uchumi wao utaombea pia na mamlaka za nchi ili uwe upate ulinzi wa Mungu kwenye hiyo biashara yako
1 Timotheo 2:2
[2]kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
 
TUOMBE:

Baba katika jina la Yesu Kristo, tunasogea mbele zako asubuhi ya leo, tukisema asante kwa ajili ya ulinzi wako, umetulinda usiku kucha hata umetupa neema ya kuamka tena, sifa na utukufu zikurudie wewe.

Tunasogea mbele zako kwa ajili ya wenzetu ambao ni wagonjwa, wengine wako mahospitalini wamelazwa nguvu ya uponyaji ikapita kwa ajili yao, ninakataa roho za mauti katika jina la Yesu ziwaachie, wapate afya sawa sawa na mapenzi yako, nina wakumbuka watoto wako wenye shida mbali mbali wengine wako kwenye misiba Baba ukawe mfariji wao, yatima na wajane ee Mungu ni nakusihi uwatunze maana umesema wewe ni Mume wa wajane, Baba wa Yatima, katikati ya magumu wanayopitia ukawe pamoja nao.

Ninaomba kwa ajili ya kazi zetu mbali mbali ukazibariki, kwenye Biashara unasema wewe ni Mungu utufundishaye kupata faida, Katika Jina La Yesu tukapata faida, wengine wameajiriwa Mungu ukawasaidie katika maeneo yako ili utukufu wako ukajidhihirishe. Nimeomba hayo machache, kwa jina la Mwanao mpendwa Yesu kristo ninaomba na kushukuru. Amen
 
Marko 11:23-25

[23]Amin, nawaambia, Ye yote atakayeuambia mlima huu, Ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake.

[24]Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

[25]Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
 
Isaya 65:23-24

[23]Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.

[24]Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
 
Amina
 
Mwenyezi Mungu, muumba wa mbingu na nchi, ninainua roho yangu kwa ibada ya unyenyekevu na sifa kwako. Ninajua kuwa kila zawadi nzuri na kamili inatoka kwako, kwa hivyo nakuomba mafanikio leo. Neno lako linaahidi, “Mkabidhi Bwana kila ufanyalo, naye ataitimiza mipango yako”
Mithali 16:3
Mkabidhi BWANA kazi zako,
Na mawazo yako yatathibitika.

Mithali 16:4
BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake;
Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya.
 
Bwana Yesu asifiwe
Ni siku nyingine tena Mungu ametupa kibali Cha kukutana wale wote wenye changamoto za kiafya Mungu awafanyie wepesi
Ni siku nyingine tena tunakutana hapa jukwaani bado tunaendelea kuombea kazi zetu na vipawa vyetu ili tukaendelee kustawi zaidi
 
Qur'an 1:1. KWA JINA LA MWENYEEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU 1

2. Sifa njema zote ni za Mwenyeezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; 2
3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; 3
4. Mwenye kumiliki siku ya malipo. 4
5. Wewe tu tunakuabudu, na wewe tu tunakuomba msaada. 5
6. Tuongoe njia iliyonyooka. 6
7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea. 7
 
Ni jambo jema mpendwa maombi yako unayotaka Mungu akutendee ukawa umeyaandika kwenye note book ili utakapotendewa miujiza utajua jambo lipi umetendewa
 
Baba wa Mbinguni, Asante kwa baraka ya kazi hii. Ninajitolea siku hii ya kazi kwako. Ninakualika, Yesu, uwe pamoja nami siku hii yote. Naomba nitekeleze kila kazi ninayokutana nayo kwa kadiri ya uwezo wangu; Nisaidie kuwa mtu mwadilifu katika yote ninayosema na kufanya.

Mithali 3:5
Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,
Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
 
Bwana Yesu asifiwe
Kesho tutakuwa na maombi ya ulinzi wetu dhidi ya maadui zetu na pia tutakuwa maombi ya kuombea baraka na mafanikio karibuni wote kwaajili ya sala na dua
 
Mungu wa mbinguni Baba mpendwa
Ninakuja kwenye kimbilio Lako kwa furaha kwa kuwa Umenilinda dhidi ya mashambulizi ya shetani.
Ee BWANA, unilinde na hila ya adui, Uniokoe na hila zake mbaya.”

Danieli 6:10
Hata Danieli, alipojua ya kuwa yale maandiko yamekwisha kutiwa sahihi, akaingia nyumbani mwake, (na madirisha katika chumba chake yalikuwa yamefunguliwa kukabili Yerusalemu akapiga magoti mara tatu kila siku, akasali, akashukuru mbele za Mungu wake, kama alivyokuwa akifanya tokea hapo.

Isaya 54:17
Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema BWANA
.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…