Uzi maalumu kwaajili ya maombi ya Alfajiri

Mungu uliye mkuu,tunakuombea waja wako,tumeamka asubuhi hii tujalie ridhiki zetu kama upendavyo,tusitishe Salama siku ya Leo,tupe Amani ya mioyo,tulinde na mabaya yote Tunaomba na Kushukuru .Amina.
Nani alikudanganya kuwa ukiomba mabaya hayatokei?
 
Ameni
 
Amina
 
Tunakushukuru Mungu sana kwa siku ya leo.


Siku ya leo Mungu akakuinue na kukujalizia pale ulipopongukiwa , pia akapate kuubariki na kuupa Afya mwili wako wa damu nyama na mifupa. na mwisho Bwana ukatende Kwa viongozi wetu kawape hekima ndani yao ya kutuongoza vyema

Na wale walio-vifungoni magerezani kawajaze tumaini na wagonjwa mahosptalini kawape uzima wa rohoni na mwilini.

Na Hili likawe ombi langu kwako Mungu wangu



 
Dear Lord, This morning as I contemplate a new day, I ask you to help me. I want to be aware of your spirit.... leading me in the decisions I take, the conversations I have, and the work I do. I want to be more like you, Jesus, as I relate to the people I meet today.... friends or strangers
 
Maombi ya kumjua Mungu zaidi

Bwana, tafadhali nisaidie kukujua wewe zaidi
Ninajua kwamba Wewe huna kikomo
Ninatazamia kwenda ndani zaidi na wewe siku baada ya siku
Ninashukuru sana kwamba
Unanipenda na unataka uhusiano nami
Nisaidie niendelee kukutafuta maisha yangu yote na ubariki juhudi zangu za kukujua Wewe
Katika jina la Yesu Amina

Soma neno na kushika
Waefeso 1:18
macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
Yohana 15:5
Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

Wimbo mzuri wa kusifu na kuabudu kutoka kwa Boaz utakubariki san usikilize
 

Attachments

Jambo la muhimu wapendwa maombi yaende sawa na usomaji wa Neno biblia kila siku itakusaidia sana ikiwa unafanya maombi ya kuomba uponyaji fungua biblia tafuta vifungu vyote vinavyozungumzia uponyaji soma na ushike neno lisitoke kinywani mwako unaposoma neno na kulishika unakaribisha Ile nguvu ya Roho Mtakatifu huyu Roho Mtakatifu atakupeleka katika viwango vingine vya juu sana vya kufanya maombi na Bwana Yesu ataachilia hitaji lako ili upone
 
Tufanye maombi bila kubagua dini

Hata Waisilamu wanakaribishwa tusibague.
 
Admin ungeweka time table itakayokuwa inatuongoza katika kujifunza neno na maombi ambayo tunayotakiwa tunayafanye kuanzia jumatatu mpaka jumapili itasaidia sana kwa sisi wote kila leo tunapokutana hapa tujue tunaombea mambo gani kwa pamoja Roho Mtakatifu ananisemesha kuwa watu wengi watakombolewa kupitia jukwaa hili
 
Amkeni katika maombi. LEO, kuombea yaliyo magumu kwetu; Yeremia 32:27
Tazama mimi ni Bwana. Mungu wa wote wenye mwili. Je Kuna Neno gumu lolote nisilo liweza?
Karibu tumwendee Mungu Asubuhi ya Leo tukiamini kuwa katika yote tutakayo mpelekea anaweza na atatenda. Karibu Kwa maombi ubarikiwe mtumishi wa Bwana.

 
Hakika,
Hamna gumu linaloshindana na Mungu.

Siku ya Leo ikawe Baraka kwetu.

Ameen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…