Imeelezwa.SIMBA imepanga kumununua beki wa kulia wa Kagera Sugar, Dickson Mhilu atakayekuja kuwa mbadala wa mkongwe Shomari Kapombe.
Huyo ni beki wa pili kutajwa kuja kuchukua nafasi ya Kapombe, mwingine ni David Kameta anayecheza kwa mkopo Geita Gold ambaye amepangwa kurejeshwa Simba.
Simba hivi karibuni ilitangaza kuachana na Kameta mwishoni mwa msimu huu kabla ya Azam FC na Geita kuwania saini yake.
Simba imepanga kununua mkataba wa miaka miwili alionao beki huyo pale Kagera Sugar.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, uongozi umepokea majina mawili ya wachezaji wanaocheza nafasi hiyo ya beki wa kulia ambaye ni Dickson na Kameta kati ya hao mmoja atapewa mkataba wa miaka miwili.
Aliongeza kuwa Simba itatakiwa kuvunja mkataba wa miaka miwili kwa Dickson alionao Kagera Sugar unaomalizika 2024 huku Kameta akisaini kama mchezaji huru, kwani mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.
“Kama jina la Dickson likipitishwa rasmi viongozi, basi Simba tutatakiwa kutumia fedha nyingi kuuvunja mkataba wake wa miaka miwili utakaomalizika 2024 Kagera Sugar.
“Lakini kama akipitishwa Kameta, basi huyu tutamsajili kama mchezaji huru kwani mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu,” alisema mtoa taarifa huyo.