R Mbuna
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 2,283
- 5,371
Mkuu kwenye hili natoa ushuhuda.Usingekopi na kupesti ingependeza zaidi, nitazungumzia hapa mti ambao huzaa matunda yanayofanana na jamii za kunde japo yenyewe ni marefu zaidi, mbegu zake ni dawa, majani yake ni chakula na dawa nzuri sana pia, mti huu ni mlonge(mti wa maajabu).
Endapo utatumia majani yake kila siku utazisahau dawa za hosipitali, huu si utani.
My wife alikuwa na PID tena Kwa miaka Zaidi ya mitatu. Tulihangaika Sana hospitals bila mafanikio.
Sasa yeye yupo kwenye vikundi vyao vya kina mama wakamshauri atumie mlongo na vitungui swaumu Kwa kumeza.
Alimeza Kwa muda wa siku 15 Jana nilimpeleka TMJ wamempima tena Hana PID yaani doctor anasema hakuna hata dalili za PID.
Wakati nilitumia hela nyingi Sana Kwa matibabu ya hospitals . Ila mlonge ninao nyumbani ni kuchuma na kuchemsha Tu maji. Vitungui swaumu bei yake inajulikana.
Tunadharau hizi tiba asili Ila zinasaidia Sana.