Mimi nilikuwa muhanga wa tatizo hili kwa zaidi ya miaka kumi, Nikaponea You tube kwa mdada fulani alikuwa anafundisha tiba simple sana.
Chukua Colgate ile dawa ya mswaki, Kisha chukua maji ya limao na mafuta ya nazi, changanya hadi upate mchanganyiko mzuri. Vipimo iwe ni ujazo sawa kwa kila kimoja. Kisha nyoa ndevu zako vizuri then upake kwa siku saba. Vipele vyote vitaisha. After that kila ukinyoa uwe unaitumia hiyo kama after shave yako kwa ile siku ambayo umenyoa na asubuhi yake. Ukipaka unakaa nayo dakika ishirini hadi nusu saa then unaosha kwa maji safi ya moto.
Mi nimetumia na nimepona kabisa mapele sumbufu ya ndevu. Kumbuka kila unapotumia uitengeneze upya. So unapotengeza iwe ni kidogo tu ya kutosha muda huohuo. Vipimo unaweza tumia nusu kijiko cha chai kwa kila moja au kijiko kimoja cha chai kwa kila kiungo.