Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Uzi maalumu wa Mimea Tiba inayotuzunguka majumbani

Naam. Kweli ni dawa ya chunjua (Warts)na unatakiwa uitumie kwa uangalifu - huku ukimshukuru Mungu kwa kuumba mti huu. Asante.
Majani ya mti huu yaliyodondoka yenyewe kwa kukomaa na yakakauka yenyewe hapo chini ya mti , Hii pia ni dawa nzuri mno kwa tiba ya meno yanayodondoka hovyo e.g. jino linalegea bila maumivu halafu baadaye linang'ooka lenyewe au muathirika anaamua kulitoa kutokana na usumbufu anaoupata wakati wa kula chakula.
 
Majani ya mti huu yaliyodondoka yenyewe kwa kukomaa na yakakauka yenyewe hapo chini ya mti , Hii pia ni dawa nzuri mno kwa tiba ya meno yanayodondoka hovyo e.g. jino linalegea bila maumivu halafu baadaye linang'ooka lenyewe au muathirika anaamua kulitoa kutokana na usumbufu anaoupata wakati wa kula chakula.
Ya natumika je hayo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Historia ya Binadam imetokana na mnyama, ulikuwa zamani unakaa misituni huko unakula mimea na mizizi hayo madawa ambayo yana chemical futilia mbali.

BURE kabisa, "dawa ya UTI nakupa warranteee!!! wa miaka 7 bila UTI nyumbani mwako

Chukua majani ya mchungwa vikombe 4, yaoshe yachemshe na mizizi yake au magombe jikoni

Tenga mezani kikombe kimoja tia kijiko kimoja cha chapa maandazi kunywa vikombe 4 kwa siku

Hutaenda kununua hizo dawa za UTI najua wapo wanaouza dawa za UTI BUT hizi mimea ni haki yako mtu mweusi kuijua ndio asili yako na sisi wasomi Elimu yako itoe tija kwa watu weusi wenye vichwa vigumu kuamini Mzungu ni BORA.
Unamaanisha mzungwa?
 
Jinsi ya kujiponya bawasili

MWANZO.
Watu wengi wamekuwa wakihangaika na ugonjwa wa bawasiri bila ya mafanikio ya kupona na wengine huwapelekea kuzoea tatizo hili na kuona ni tatizo la kawaida na la mazoea limeshakuwa kuwa kwao kutokana na kukata kwao tamaa,

Yote hii husabishwa na kujitibu kwa muda mrefu bila mafanikio, lakini ukibahatika kuona darasa hili basi waweza kuwa umepona ewe mgonjwa wa tatizo hili;

Ufahamu kwanza ugonjwa huu:

Bawasiri ni ugonjwa ambao husababisha vijinyama kutoka nje ya tundu la haja hubwa na kutanuka kuunda mfumo kama wa utumbo ambao huchomoza na kuonekana ni utumbo na kiswahili watu husema ugonjwa wa kujisaidia na utumbo kutoka nje kwa kingereza huitwa hemorrhoids.

Chanzo chake:

Ugonjwa huu huja kwa vyanzo viwili moja ni kama maradhi ya hospitali na yapili ni kama maradhi ya malogo au kulogelezewa.

KAMA HOSPITALI:

Wanavyodai watu wa hospitali au watu wa science ya mwili wa mwanadamu source ya bawasili ni kama ifuatavyo:

*Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefu.

*Ujauzito – wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.

*Kushiriki mapenzi kinyume na maumbile.

*Uzee – kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.

*Sababu za kurithi – baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni asilimia ndogo sana.

*Kuharisha sana kwa muda mrefu

*Kutumia vyoo vya kukaa

*Kunyanyua vyuma vizito

*Mfadhaiko/stress

*Uzito na unene kupita kiasi nk

Hizo ni baadhi za according za wanasayansi japo still bado hawajaelewa vema where is this come from.. hii ni kwa upande wa kihospitali,

Dalili za bawasiri according to hospital:

*Maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa

*Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia

*Muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa

*Uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa

*Haja kubwa yaweza kujitokea tu muda wowote

Dalili za bawasili according to spiritual

*Ugonjwa hutokea ghafla bila dalili.

*Kutoka maji hovyo bila kipimo

*kutokwa na damu na kuvimba hilo dude hovyo na kusinyaa ghafla
kutoa malenda lenda sehemu hizo,

*haikukumbi athari zake hadi uwe mbele za watu

*usiku ukilala unaota unaingiliwa au kubakwa iwe mwanaume au mwanamke

*kuhisi wakati wa kuvuja damu kama mtu au kitu kinanyonya hapo

* kuambiwa kila aina ya dawa na kutumia zote bila mafanikio.

TIBA YAKE:
Ikiwa utatibiwa hospitali na ugonjwa umekaa muda mrefu basi itakulazimu ufikie decision ya kukubali kupasuliwa ambapo kama ni tatizo la kishirikina litapungua kwa kasi kubwa sana na baada kuanza upya kwa nguvu zaidi lakini ikiwa ni la kawaida basi ukipasuliwa ndio umepona na kupewa vidonge vya kukausha hili tatizo..

Pale ambapo litaanza tena basi jua ni mazingara yanafanya kazi na ili uweze kutibia inabidi kitu cha kwanza ujue je, bawasili uliyonayo ni ya ndani au ya nje?

Kama ni ya ndani basi kupona kwake ni ngumu kidoge na itabidi utumie dawa ambazo ukikosea kidogo zaweza kukuletea vidonda vya tumbo ila hilo tatizo litakuwa limetoweka

Na kama ni ya nje basi utawahi kupona kwa maana haya matatizo ili ulijue limekaa kimazingara lile lililotoka nje ndio lipo ndani na la ndani ni hili la nje,

Na kama ni sehemu zote ndani na nje basi hawa hutumia mwezi mzima wa kutumia dawa kuweza kupona,

Ili uweze kuharakisha kupona basi lazima ujue details zote za hilo bawasili kama urefu,upana,lilipoegemea,linavyosurvive details zote utatakiwa uniinbox ili niweze kukwambia na kusugest ni dawa ipi itakufaa hapa natoa mbili tu ya ndani na ya nje ya kwa lile linaloanza kupeya,, yaani lenye miezi minne hadi sita kwa urefu wa nchi 2 na upana wa mdomo wa chupa ya energy ya azam.

DAWA
chukua ubongo wa jogoo mwekundu yule mwenye sharubu na nyongo yake vichanganye pamoja na uviweke kwenye chupa ndogo ya mafuta mazito yale baby care kisha tia humo chumvi,mafuta ya nyonyo na siki ya vinegar ya zabibu,
koroga hadi ibaki rojo ndio itakua mafuta ya kuchua kutwa mara mbili

Kisha chukua
Kitunguu swaumu, pilipili manga,tangawizi na chumvi vijiko vitatu vitatu kisha uchanganye na Asali nusu lita vitunguu vitano vya swaum.. utakunywa asubuhi kabla hujala kitu na jioni..

wiki mbili hilo tatizo linabaki hadithi ya kale kwako.

Pia ukiitaji dawa hii ya bawasili iliyo tayari zipo kalibuni.
 
Asalam alaykum habar za masiku,naam baada ya kupotea sana kwa mda mrefu kutokana na majukum ya Kaz kunibana hatimae leo nimerejea Tena na kigongo iki kama zawad yangu kwenu

KUMVIMBISHA MWIZI TUMBO Ikitokea mmoja wenu ameibiwa ama amedhalilishwa na jambo fulani basi usijali chukua njegere nyeusi na uzitie kwenye beseni tia na maji ujazo kulingana na njegere zako ila zinatakiwa njegere zielee kwaiyo swali sunat rihaja na utamswalia mtume X 100 utaanza na astaghafiru x100 utamaliza na ya MUMITU X313 Baada ya hapo sema unataka alie kuibia labda cm ama pesa au chochote kile basi kisikike tumboni mwake kikilia na tumbo limvimbe kama mama mjamzito unatakiwa kusoma ABJADI X1001 na kila ukifika mala 100 utasoma ALAMTARA utakomea panapo sema kaaswifin kisha sema manuizi yako na huku ukiwa kidole chako cha shahada unakichezesha kwenye hayo maji uliyo tosa njegere zako ukisha maliza maji hayo usiyatupe japo kuwa ndani kwako kutatanda harufu ya uwozo ila wala usijali tafuta sehemu mzuri yahifadhi na kaa baada ya masaa3 utaona mwizi wako analetwa tena kabebwa kwenye machela😂😂😂 na ukisha ona hivyo utasikia kuwa alivyo kuibia kuwa vikilia tumboni ila uweke manuizi mfano ee mungu anomba unidhihilishie huyu alie niibia na naomba kwa kitu alicho iba naomba kikalie tumboni mwao hata kama walikuwa 100 wote watapata adhaba hiyo Na badala sasa ya kuletwa opoo lake
🤔🤔🤔🤔Apa akija nitafute nikupe opoo lake,ngoja niishie apa nisije kuwekewa bifu na dunia bureeee😂😂😂😂😛😛😛😛.
 
MVUTO WA AJABU WA BIASHARA .
DAWA KIBOKO YA MVUTO.

dawa hii ni ya miti dawa hii ni kibojo ya biashara kama wewe ni mama ntilie(muza chakula) mfanya biashara wa aina yoyote basi hili ni bomu lako ili likulipukie , hii dawa niliwai toa humu kipindi hicho na watu waliizarau kwakua hawakuniamin lakin hii nasema utaangaika nadawa za mivuto hili ni bomu kama wewe una frem, kilinge, biashara ya kutembeza , umachinga nk haki ya allah iko juu yetu wana imani nae ni mwingi wa muelevu nenda duka la asili kanunue

1LUHAHO

2MLIPU

3MCHEKA

4MWINAMO

5MVUTE

6KINAMATA.

dawa hii itumie kwa kuchoma kama sehemu yako ya biashara inaruhusu kuchoma , pakaa dawa hii kila siku asubui ila ukiwa umechanganya kwenye mafuta NAZI , ndugu yangu pakaa kwa manuizi ya mvute hata kama wewe kazin kwako hukuwai kupanda cheo basi hii ni mwisho wao utapanda , na umefukuzwa kazi alafu huelewi kuwa nini sababu basi hili ni ponyo sina mengi fanyeni ili mufaidike na nyinyi ndugu zangu🙏🏽.
 
View attachment 2388645
jinsi ya kumjua mwanamke au mwanaume aliyewekewa tego la kiganga na mpenzi wake hili asichepuke.

KWAKUTUMIA JANI LA MGOMBA.

Tumefundisha dawa nyingi za mapenzi,zikiwemo dawa za mtu kumfunga mpenzi wake wa kike ama wa kiume hili asiweze kuchepuka.

Wengine huwafunga wapenzi wao hili kama unafanya nae mapenzi upatwe na ugonjwa wa ajabu,tupu zinasane na mambo mengine mengi.
Sasa ukitaka kujua kama mtu uliyenaye amefungwa kiganga/kichawi fanya yafuatayo.
-chuma jani la mwisho kabisa kwenye kilele cha mgomba
-Jani hilo litie kwenye uvungu wa kitanda alichokaa au kulala

Matokeo.
1.ukilitia tu jani uvunguni na likasinyaa hapohapo ujue huyo hafai na atakusababishia majuto.

2.kama jani litakuwa vilevile basi ujue yuko salama endelea kuenjoy.
Science au uchawi?
 
MVUTO WA AJABU WA BIASHARA .
DAWA KIBOKO YA MVUTO.


dawa hii ni ya miti dawa hii ni kibojo ya biashara kama wewe ni mama ntilie(muza chakula) mfanya biashara wa aina yoyote basi hili ni bomu lako ili likulipukie , hii dawa niliwai toa humu kipindi hicho na watu waliizarau kwakua hawakuniamin lakin hii nasema utaangaika nadawa za mivuto hili ni bomu kama wewe una frem, kilinge, biashara ya kutembeza , umachinga nk haki ya allah iko juu yetu wana imani nae ni mwingi wa muelevu nenda duka la asili kanunue

1LUHAHO

2MLIPU

3MCHEKA

4MWINAMO

5MVUTE

6KINAMATA.

dawa hii itumie kwa kuchoma kama sehemu yako ya biashara inaruhusu kuchoma , pakaa dawa hii kila siku asubui ila ukiwa umechanganya kwenye mafuta NAZI , ndugu yangu pakaa kwa manuizi ya mvute hata kama wewe kazin kwako hukuwai kupanda cheo basi hii ni mwisho wao utapanda , na umefukuzwa kazi alafu huelewi kuwa nini sababu basi hili ni ponyo sina mengi fanyeni ili mufaidike na nyinyi ndugu zangu[emoji1431].
Hivyo vyote unavichanganya au??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom