Nimepitia habari hii Jf watu wengi wamefurahi Rais Dr Samia kuitaja Jf na kuona fahari kubwa.
Sasa tunasahau kuwa Muumba na muweza wa yote Allah aliyetakasika na yeye huwa anawataja watu na kuwasifia mbele ya kundi la wabora nao ni Malaaika ,je kuna ufahari wowote unaozidi huu wa kutajwa kwa kisifiwa na Mola mlezi mwenye utukufu wote ?
Ni watu gani hao anaowataja na kujisifia kutokana na hao ? jibu ni watu ambao humkumbuka mara kwa mara kwa kumtaja ,kukaa katika vikao vya kheri/kielimu n.k
Muda mwingi tunaupoteza mitandaoni bila faida ,vijiweni na katika mambo mengine huku tukipuuzia utajo wa Allah kituambacho ni rahisi ukikosa kutenga muda wa fatagha hata njiani unaweza kusema Alhamdullihal,SubhanaLlah pamoja na adhkar nyinginezo ...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.