Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

Uzi maalumu wa picha za nukuu na misemo mbalimbali ya kiislamu

FB_IMG_16366237173487652.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nukta muhimu.

Katika pita pita zangu sehemu mbalimbali na kukutana na watu wa aina tofauti nimegundua bado swala la Nia limekuwa likieleweka vibaya miongoni mwetu.

Ni kweli hakuna ibada inayokubaliwa pasipo kuangalia nia ya mfanyaji .Moja kati ya malengo ya nia ni kutofautisha Kati ya kufanya ibada kwa ajili ya mazoea ,watu na malengo ya kidunia na mtu kufanya kwa ajili ya kupata malipo na radhi za Allah tabaraka wataala. Vilevile kutofautisha baina ya ibada mfano funga ya Suna na faradhi ,Swala nk.

Dhana potofu kuhusu nia.
Kuna dhana imejengeka mtu kuwa na nia ya jambo fulani(la kiibada ) mfano swala ,funga nk lazima unuwie kwa sauti tena kiarabu. Hili halipo sawa na uchunguzi wangu umebaini sababu hii imepekea wengi kuacha kuanza ibada na uvivu katika ibada na kuacha baadhi ya ibada Ktk dini.Mfano

1.Kuna ndugu yangu alikua na safari fupi akachelewa kuswali swala tatu akaswali Insha tu nikamuuliza vipi nyingine umeswali akasema sijui kunuwia swala za kulipia ikiwa umepata dharura .

2.Mwingine hata kufunga nk analeta kisingizio kua hajui kunuia.

Usahihi wake upo vipi jambo hili?
Kunuia jambo ni hali ya mtu kujua anafanya kitendo gani mfano na kwa ajili ya nani au maslahi yapi na hivi vyote haziitajii au kulazimia utamke kwa sauti na iwe kiarabu.
a21193b282dd08417dd132e69b50c33d.jpg

Na imenukiliwa "Dini ya Uislamu ni nyepesi na yeyote atakayeweka ugumu kwenye dini itamshinda"
he-knows-what-is-in-every-heart-e28093-surah-mulk-67-13(1).jpg

Mfano mfupi
Let’s+practice+making+niyyah.jpg

Nb:Sijawahi kuona hadithi sehemu imeandikwa Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) alinuia hivi wakati akifanya ibada fulani.
 
Tupo katika Mwezi wa Muharam na miongoni mwa miezi mitukufu ambapo inatakiwa mtu apupie kufanya wema na ajitahidi kumcha Allah kwa kuweka kandi na kuacha maasi
88be51ebf3a17cc35d7e870050db77a6.jpg
 
"And fear a Day when you Will be returned to Allah . Then every soul will be compensated for what it earned , and they will not be treated unjust" (2:281)
 
Neno la jioni ; Hii ndio siri ya mafanikio ya mwanadamu katika maisha ya Dunia na Akhera na mafanikio sio lazima utajiri wa mali ,wana ,umaarufu ,cheo nk bali mafanikio ni kuridhika kwa moyo pamoja na kuishi katika hali ya ubora inayomridhisha Muumba wetu katika maisha haya mafupi dunia hatimaye naye Mola akuridhie wakati wa kuondoka duniani vingene ni nyongeza katika maisha yetu.

Na siri yenyewe ni neno zito na lenye hadhi kubwa kabisa
f6da11bf9efb5e713f93c83f042de6c6.jpg


Ukiamini hilo neno na kulizingatia kimaana na kiutendani kama inavyotakiwa wewe hautaiba ,hautadhulumu ,mambo ya kidunia hayokushughulisha kusahau ibada ,hauto muogopa kiumbe mwenzako ,kupapatikia kuhofia umasikini nk.

Kwani Hilo neno linaleta faraja na utulivu wa moyo kama inavyosema kwa kukubali moja kwa moja kuwa wewe si kitu na hata ukifeli(hali ya kuwa umepambana) usijilaumu wala kuchukua maamuzi ya kijinga mfano kutumia vilevi kuondoa mawazo kwani unaamini kuwa uwezo wote ni wake Allah na yeye anakujua zaidi na huenda **** makubwa mazuri mbeleni au umeepushwa na jambo la hatari usilolijua

Hivyo ni vyema kuelewa tamko hili na kuzidisha kulitaamka kwani kila ukitamka unaandikiwa wema katika kitabu chako cha matendo na ndio maana Mtume Muhammad (upon him be peace and blessing of Allah) amesema hili neno ni hazina ya peponi vilevile na hadithi nyingi zinaeleza ubora wa mtu kudumu na neno hili na kuzidisha kulitaamka.
tumblr_npfyszpFUp1s23ywwo1_1280.jpg
 
Back
Top Bottom